Meli za jeshi la Marekani zapita katika mlango-bahari wa Taiwan

Marekani imepitisha meli zake za kijeshi katika Mlango-bahari wa Taiwan, katika hatua za jeshi la nchi hiyo kuendeleza shughuli katika eneo hilo la kimkakati licha ya upinzani mkali kutoka China.

Taarifa ya jeshi la Marekani imesema hatua hiyo ilikuwa na lengo la kudhihirisha msimamo wa Marekani kuhakikisha uhuru wa safari katika ukanda wa bahari ya Hindi na Bahari ya Pasifiki.

Aidha, katika taarifa hiyo, Marekani imesema itaendelea kupeleka ndege zake na meli zake popote pale panaporuhusiwa kisheria.

Msafara huo wa meli za Marekani unatazamiwa kuzidisha mvutano kati yake na China, ambayo mnamo siku za hivi karibuni imekuwa ikiongeza shinikizo dhidi ya kisiwa cha Taiwan ambacho inashikilia kuwa ni himaya yake.

Hata hivyo, utawala wa kisiwa hicho ambao utaikaribisha hatua hiyo ya Marekani, kama uungaji mkono wakati mvutano ukishamiri kati yake na Serikali ya mjini Beijing.


from MPEKUZI

Comments