Waziri Mkuu Aridhishwa Na Hatua Za Ujenzi Wa Teminarl III katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kusema ameridhishwa hatua iliyofikiwa.
 
Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, mwaka huu ambapo hadi sasa tayari maeneo mengi yamekamilika ikiwa ni pamoja na sehemu za abiria wanaowasili na kuondoka.

Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo jana (Alhamisi, Februari 28, 2019) amesema amefurahi kukuta michoro ya wanyama kama tembo, twiga, bahari, minazi na majahazi ambayo ni alama za nchi.

Kufuatia kukamilika kwa uwanja huo kwa asilimia 95, Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ianze kukamilisha  taratibu za kuutumia uwanja huo ili mkandarasi anapoukabidhi uanze kutumika.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameipongeza kampuni inayojenga uwanja huo kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa sababu jengo ni zuri na linavutia. Pia amewapongeza Watanzania wanaofanya kazi kwenye mradi huo.

Awali, akisoma taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa Walaka wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale alimuelezwa Waziri Mkuu kuwa jengo hilo limekamilika kwa asilimia 95.

Mhandisi huyo alisema tayari wamefanya majaribio ya kwanza ya mifumo na vifaa mbalimbali na kwamba mkandarasi anatarajia kukabidhi mradi huo Mei 31 mwaka huu. Jengo hilo linauwezo kubeba abiria milioni sita.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


from MPEKUZI

Comments