PICHA: Lowassa Afika Nyumbani kwa Ruge Mutahaba Kutoa Pole na kuwafariji wafiwa.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa leo asubuhi wamefika nyumbani kwa Prof. Mutahaba ambaye ni baba mzazi wa Ruge Mutahaba aliyekuwa mkurugenzi wa uzalishaji vipindi wa Clouds Media Group kutoa pole na kuwafariji wafiwa.

Ruge Mutahaba Alifariki dunia Juzi nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu ya figo zilizoanza kumsumbua mwaka jana. 

Mwili  unatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam kutokea Afrika Kusini siku ya kesho Ijumaa, Machi 1, 2019.


from MPEKUZI

Comments