Mrisho Mpoto Avunja Ukimya......Amtaka Diamond Ahudhurie Msiba wa Ruge Mutahaba

Msanii wa muziki wa asili nchini Tanzania, Mrisho Mpoto, maarufu kama ‘Mjomba’ amemtaka msanii mwenzake, Diamond Platnumz asikae kimya na badala yake  ahudhurie katika msiba wa  Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba

Mrisho Mpoto kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika kwa majonzi akisema; “@diamondplatnumz Nasib Abdul nimekwita jina lako la kuzaliwa mimi kama kaka yako unaeniheshimu na kunisikiliza nakwambia. RUGE MUTAHABA AMEFARIKI nakuomba NJOO UMZIKE… Nimemaliza.”

Msanii Diamond  amekuwa kimya mpaka sasa, si kuposti mitadaoni au kufika msibani jambo ambalo limeibua maneno.

Hivi karibuni, ilidaiwa kuwa Diamond na Lebo yake ya WCB waliingia kwenye bifu zito  na Ruge Mutahaba kwa madai ya kutofautiana katika mambo yao ya sanaa.


from MPEKUZI

Comments