India na Pakistan zimesema kila mmoja imetungua ndege za kivita za mwenzie , siku moja baada ya ndege za kivita za India kushambulia ndani ya Pakistan kwa mara ya kwanza tangu vita vya mwaka 1971, na kusababisha mataifa makubwa duniani kuzitaka nchi hizo kuonesha uvumilivu.
Nchi zote zimeamuru mashambulizi ya anga katika nchi hizo, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ambapo nchi hizo zenye silaha za kinyuklia kufanya hivyo, wakati majeshi ya ardhini yameshambuliana katika maeneo zaidi ya kumi na mbili.
Hali ya wasi wasi imeongezeka tangu pale shambulio la kujitoa muhanga katika gari lililofanywa na wanamgambo kutoka Pakistan na eneo la Kashmir linalomilikiwa na India kuwauwa kiasi ya wanajeshi 40 wa India hapo Februari 14, lakini kitisho cha mzozo kiliongezeka haraka jana wakati India ilipoanzisha mashambulizi ya anga katika kile ilichosema ni kituo cha mafunzo ya wanamgambo.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment