Dudu Baya Ajisalimisha Polisi

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema msanii, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi Oyster Bay jijini Dar es Salaam kwa mahojiano kutokana na tuhuma za kukashifu na kutoa lugha za kejeli kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, marehemu Ruge Mutahaba.

Dudu Baya amejisalimisha leo Februari 28, 2019 baada ya kuamriwa na Baraza la Sanaa la Taifa kufanya hivyo.

Jana, Waziri wa Habari na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe aliagiza Jeshi la Polisi na Basata wamchukulia hatua mwanamuziki huyo kwa makosa ya kumkashifu, aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji, Ruge Mutahaba.

Baada ya amri hiyo, Basata ilimtaka mwanamuziki huyo kujisalimisha katika kituo cha polisi Oysterbay asubuhi ya leo.


from MPEKUZI

Comments