BREAKING: Freeman Mbowe na Esther Matiko Washinda rufaa ya dhamana yao dhidi DPP

Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali pingamizi la Serikali kupinga Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko kusikilizwa shauri lao la kuomba kupewa dhamana katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam

Hivyo kesi ya Mh. Mbowe na  Matiko inarudi Mahakama kuu kwa ajili ya kusikilizwa kama ilikuwa halali kwa Hakimu kufuta dhamana zao au hapana.


from MPEKUZI

Comments