Kamati ya Bunge yashauri viwango vya adhabu na vifungo Barabarani Vipunguzwe

Kamati ya Bunge ya Miundombinu imeshauri kupunguza viwango vya adhabu na vifungo katika Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti na Usafiri wa Ardhini wa mwaka 2018.

Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo bungeni leo Jumatano Januari 30, 2019, mjumbe wa kamati hiyo, Dk Chuachua Rashid ameshauri viwango vya adhabu na vifungu kupunguzwa ili kuendana na hali halisi.

Amesema kamati hiyo inashauri katika kanuni kuwe na kikokotoo kinachotokana na gharama ya uendeshaji ili kutatua changamoto hiyo.

Kamati hiyo pia imeshauri magari makubwa ya mizigo nayo yafanyiwe utaratibu wa kufungwa kidhibiti mwendo kwa sababu imebainika hivi karibuni kuwa ajali nyingi zimekuwa zikisababishwa na mwendo wa kasi wa malori.


from MPEKUZI

Comments