Ujenzi wa Mji wa serikali kumeendelea kuwanyima usingizi viongozi na watendaji mbalimbali wakiwemo mawaziri.
Pia, serikali imetishia kuwanyang’anya zabuni ya upelekaji kokoto kwenye mji wa serikali Ihumwa baadhi ya kampuni za uzalishaji kutokana na kusimamisha uzalishaji kwa madai kuwa watendaji wake wapo likizo.
Uamuzi huo ulitolewa jijini hapa jana na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye viwanda vya kuzalisha kokoto vya kampuni ya Laroy Aggregates na WADI akiwa ameambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde.
Katika ziara hiyo, viongozi hao walikuta viwanda hivyo havizalishi kokoto licha ya kuwa na zabuni ya kupeleka kwenye kandarasi zinazojenga majengo ya Wizara mbalimbali kwenye mji huo.
Hatua hiyo ilisababisha mawaziri hao kuwasiliana kwa simu na wamiliki wa kampuni hizo na kuwapatia maelekezo kuhakikisha ifi kapo Januari 3, mwakani wawe wameanza uzalishaji ili kuharakisha ujenzi wa mji huo.
Katika hatua nyingine, serikali imewataka watu wote wenye leseni za uchimbaji wa kokoto katika eneo la Chigongwe jijini Dodoma kuhakikisha wanafanya uzalishaji kwa kuwa serikali haitasita kuzichukua leseni hizo.
Naibu Waziri Biteko alisema wametembelea wazalishaji hao kutokana na ziara iliyofanywa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika mji huo ambapo aliagiza ujenzi uende kwa kasi.
Alifafanua kwamba wakandarasi wanaofanya ujenzi katika mji wa serikali wanalalamika wazalishaji kokoto hawapeleki za kutosha na kusababisha ujenzi kutokwenda kwa kasi inayotakiwa, hivyo wameamua kutembelea ili washuhudie, ambapo wamekuta wengi wameenda kwenye mapumziko.
“Viwanda hivyo vimechukua zabuni Shirika la nyumba(NHC),
Shirika la Mzinga na kandarasi nyingine zinadai kokoto kwa ajili ya ujenzi huo. Cha kushangaza hawa ambao tumewapatia oda wameenda likizo wakati wajenzi wapo ‘site’ wanasubiri kokoto, tumeenda kwingine tumekuta mitambo ni mibovu inahitaji matengenezo,”alisema.
Biteko aliagiza wale wote waliopewa leseni za uchimbaji wafanye kwa weledi mkubwa na wale ambao hadi kufi kia tarehe hiyo watakuwa hawajaanza uzalishaji wa kokoto na kupeleka mchanga zabuni zao zitachukuliwa na kupewa kampuni nyingine nje ya Dodoma yatakayokuwa tayari kupeleka kokoto.
Alisema ujenzi huu unatakiwa kufanyika kwa kasi na kuwataka watu wote ambao hawafanyi vizuri watawafutia zabuni na kuwapatia watu wa Lugoba na Chalinze ambao wana uwezo wa kuzalisha na kukidhi mahitaji ya wakandarasi.
Naye, Naibu Waziri Mavunde alitoa rai kwa wazalishaji kuhakikisha wanakidhi matarajio ya ujenzi wa mji huo kwa kuwa ni fursa kwa watu wa Dodoma.
“Watu wa Dodoma tufanye kazi kwa weledi ili fursa tuliyokuwa tunaililia iweze kukidhi mahitaji kwa kuwa kuna mahitaji makubwa ya kokoto,” alisema.
Ofisa Madini Mkoa wa Dodoma, Jonas Mwano alisema atahakikisha anafuatilia kila siku kwa viwanda hivyo ili kukidhi
mahitaji ya ujenzi wa mji huo.
“Ofi si yangu imetoa leseni 75 za uchimbaji kokoto katika eneo la Chigongwe, nawataka wale wenye leseni waanze kuchimba ili kuongeza uzalishaji na wale ambao hawataweza
tutazichukua na kuwapa watu ambao wapo tayari kuanza uzalishaji,”alisema.
Alisema awali walisingizia soko lakini hivi sasa soko ni kubwa Dodoma kutokana na miradi mbalimbali ya ujenzi inayofanyika.
Ziara hiyo ilikuja siku chache baada ya Waziri Mkuu kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali na kukuta ujenzi ukisuasua.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika machimbo ya kokoto ya kampuni ya Laroy Aggregate Co. Ltd, Kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthon Mavunde na kushoto ni msaidizi wake Kungulu K. Masakala
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko, akitoa tamko la Serikali kwa wachimbaji wa kokoto alipofanya ziara kujionea kinachoendelea katika machimbo hayo baada ya kubainika uhaba wa kokoto katika eneo la ujenzi wa ofisi za Serikali Ihumwa jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthon Mavunde (Kulia) wakiangalia moja ya kifaa kinachotumika katika kuchoronga mawe kwa ajili ya kokoto ambacho kwa sasa hakifanyi kazi kutokana na kuharibika. Katikati ni Fundi wa mashine katika mgodi wa WADI Gao Peng
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment