MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru amesema uongozi wa hospitali hiyo utachukua hatua za kinidhamu mtumishi atakayejihusisha na vitendo vya rushwa na kutoa lugha chafu kwa wateja.
Haya aliyasema jjini Dar es Salaam juzi wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya Serikalini (TUGHE), tawi la Muhimbili.
Alisema, kuwa mtumishi wa umma anapaswa kuwa mfano katika kutoa huduma bora na kuzingatia nidhamu.
Prof. Museru alisema endapo itabainika kwamba mtumishi kujihusisha na vitendo hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ili iwe fundisho kwa wengine.
“Jina la Muhimbili liendelee kuwa safi tusikubali watu wachache watukwamishe ni lazima tushirikiane katika kuwafichua watu hao ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao,” alisema Prof. Museru.
Aliongeza kuwa, hospitali hiyo imekua ikiendelea kuboresha huduma zake na kufanikiwa kuanzisha huduma za kibingwa ambazo awali zilikua hazifanyiki nchini.
“Tumeanzisha huduma ambazo zamani ilikua ni lazima mgonjwa aende kutibiwa nje ya nchi, na vilevile tunatoa huduma ya tiba radiolojia (Interventinal Radiology), nia yetu ni kuhakikisha huduma hizi zinaendelea ili Watanzania wengi wazipate,” alisema.
Alieleza kuwa sasa huduma hizo wanaitoa Muhimbili, ambapo wanatoa huduma ya kupandikiza figo ambapo mpaka sasa wagonjwa 28 tayari wamepandikizwa, watoto 21 wamewekewa vifaa vya kusaidia kusikia (Cochlear Implant).
Mbali ya huduma hizo, Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa kwa sasa wanafunga MRI mpya ili kuipumzisha iliyopo ambayo imefanya kazi kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Katibu wa TUGHE Mkoa wa Ilala, Tabu Mambo aliupongeza uongozi wa Muhimbili kwa utendaji bora wa kazi na kueleza kuwa chama hicho kinatambua mchango mkubwa unaotolewa na hospitali hiyo katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.
Mkutano huo ulibeba ajenda mbalimbali ikiwemo kutoa taarifa za utendaji kazi wa chama pamoja na kutoa taarifa ya mapato na matumizi kwa mwaka
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment