Msanii wa muziki Bongo, Alikiba amweka wazi kuwa atafanya show mbili za kufanga mwaka Dar es Salaam.
Moja ya show hizo mbili atakuwa na muimbaji Yvonne Chakachaka kutoka Afrika Kusini.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram jana Novemba 29 aliandika.
"Ikiwa leo ni siku yangu ya kuzaliwa namshukuru Mungu kwa kuendelea kunibariki katika kila jambo na namshukuru kwa kunipa mashabiki wanaonipa support ya dhati kabisa. Shukrani zangu kwa mashabiki mwaka huu katika #FungaMwakaNaKingKiba zinakuja na show mbili kubwa ndani ya December 2018.
1st Edition ya Funga Mwaka Na King Kiba nitakuwa na Princess of Africa Mama Yvonne_ ChakaChaka itafanyika Serena Hotel Dar es salaam 22. December. 2018.
Halafu 2nd Edition ya Funga Mwaka Na KingKiba itatukutanisha pale Next Door Arena, Dar es Salaam tarehe 29. December.2018."
Nyimbo za Yvonne zilizotamba ni pamoja na I’m Burning Up, Thank You Mister DJ, I Cry for Freedom, Makoti, Motherland, Umqombothi na nyinginezo.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment