Waziri aomba radhi kuvuja kwa picha zake za ngono

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika ya Kusini , Malusi Gigaba ameomba radhi mara baada ya video yake ya ngono kuvuja mtandaoni.

Waziri Gigaba amesema kuwa video hiyo ilirekodiwa kwa ajili ya matumizi binafsi ya yeye na mke wake ambapo video hizo zilivuja mara baada ya simu yake kudukuliwa na wahalifu wa mtandaoni mwaka jana.

Amesema video hiyo ilianza kusambaa mara baada ya wahalifu hao wa mtandaoni kumtaka atoe kiasi cha fedha alipochaguliwa kuwa Waziri wa fedha mwaka 2017.

Tayari taarifa juu ya wahalifu hawa zipo mikononi mwa sheria, hivyo uchunguzi wa kina unaendelea kufanyika.

Gigaba ameomba radhi kwa umma pamoja na familia yake hasa watoto wake, mama yake na mama mkwe wake kwa machungu na aibu kali aliyoisababisha kutokana na kusambaa kwa video yake akiwa faragha.

“Mke wagu na mimi tumesikitishwa na video hiyo ya ngono ambayo tulikuwa tuione sisi wawili tu kwani mawasiliano yangu ya simu yalidukuliwa mnamo 2016/17 na sasa inazungushwa miongoni mwa wanasiasa.

“Nachukua fursa hii kuomba msamaha kwa watu wengine wa familia yangu, hususan wanangu, mama yangu na wakwe zangu na wananchi wa Afrika Kusini kwa matatizo yatokanayo na jambo hili,” amesema Gigaba.

Katika video hiyo ya sekunde 13, Gigaba yuko peke yake akichezea uume wake kwa mkono na akisema: “Fikiria hiki kingekuwa mdomoni mwako.”


from MPEKUZI

Comments