Naibu Waziri Wa Maliasili Na Utalii, Mhe Japhet Hasunga Awashauri Wasanii Wanaopiga Picha Za Uchi

Na Lusungu Helela.
Naibu  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga  amewashauri wasanii wanaopiga picha za utupu waache kupiga picha hizo badala yake watembelee Hifadhi za Taifa ili wakapige picha na simba, twiga chui pamoja na sokwe kwa ili  waweze kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Pia amewataka wasanii wenye nia ya kutaka kutengeneza filamu  katika Hifadhi ya Taifa wawasaliane na Uongozi wa Hifadhi za Taifa au wawasiliane na  yeye mwenyewe moja kwa moja.

Ametoa rai hiyo wakati  akifunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam

Aidha, Ameiasa jamii iitumie mitandao ya kijamii kujipatia elimu badala ya kusambaza picha ambazo ni kinyume cha maadili ya Mtanzania.

Ameongeza kuwa Jamii iwakemee wasanii wenye tabia hiyo badala ya kusubilia Serikali ndo ichukue hatua.


from MPEKUZI

Comments