Jela Miaka 20 Kwa Kukutwa na Miguu Miwili ya Nyumbu Yenye Thamani ya Milioni 1.4

Mkazi wa kijiji cha Tamukeri wilayani Serengeti,Marwa Kisiri (19), amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na miguu miwili wa nyumbu yenye thamani ya sh. milioni 1.4

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya  ya Serengeti, Ismael Ngaile katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 98/2018, amesema mshtakiwa atatumikia kifungo hicho baada ya kutiwa hatiani.

Mwendesha mashitaka wa Jamhuri, Emmanuel Zumba amesema mshtakiwa alikamatwa Agosti 18, 2017 katika korongo la Tamukeri ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.


from MPEKUZI

Comments