CCM Yasema Mwisho wa Kuwapokea Wanaohamia Toka Vyama Vungine ni Novemba 15....Tazama Hapa Maamyzi ya Kamati Kuu

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewapitisha makada wake wanne kuwania nafasi ya ubunge katika maeneo yao kufuatia kikao cha kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kukutana leo jijini Dar es salaam.
 

CCM imewapitisha waliokuwa wabunge wa maeneo hayo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), waliotangaza kujiunga na chama hicho kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

Wabunge hao waliopitishwa ni Pauline Gekui wa jimbo la Babati, James Milya jimbo la Simanjiro, Joseph Mkundi Jimbo la Ukerewe, na Marwa Ryoba ambaye atawania nafasi ya ubunge jimbo la Serengeti.

Aidha Chama hicho kimetaja tarehe 15 novemba kuwa ndio tarehe ya mwisho kwa Chama hicho kuwapokea maombi ya wenye nia ya kujiunga na Chama hicho na kupewa dhamana ya uwakilishi kupitia tiketi ya CCM kwa wabunge na madiwani kutoka vyama vingine.

Aidha taarifa hiyo imesema baada ya tarehe hiyo hakuna kiongozi yeyote atakayepewa nafasi ya kugombea uwakilishi wa Chama hicho katika uchaguzi wa marudio badala yake watakuwa wanachama wa kawaida.



from MPEKUZI

Comments