AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 130 na 131 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA       

Kidogo nikajikuta nikishusha pumzi nikimshukuru Mungu kusikia kwamba Hawa hato jihusisha kabisa na oparesheni hii.
“Sawa mrs Dany ni maelekezo yapi hayo?”
“Kwa sasa siwezi kuyatoa, hadi niweze kuwa katika sehemu salama na ya kuaminika”
“Sehemu gani unahitaji kuwa Mrs Dany?”
“Ninahitaji kuishi kwa kipindi chote cha hii oparesheni ya mume wangu hapo ndani ya ikulu yako, naamini Dany atakuja kunichukulia hapo akimaliza kazi yake.”
Maeno ya Hawa yakatufanya mimi na meja kutazamana kwani sikutegemea kama Hawa anaweza kuomba kuishi katika ikuli ya raisi wa Marekani, ambayo inasifika sana kwa kuwea kulindwa kuliko ikulu yoyote Duniani.
   
ENDELEA   
“Hilo halina shaka mrs Dany, je kuna jingine zaidi?”
“Hapana ninashukuru muheshimiwa raisi kwa kuweza kunielewa”
 
“Sawa mpatie simu Dany”
Nikaichukua simu na kutoa loudspeaker, nikaiweka sikioni kwa ajili ya kumsikiliza muheshimiwa raisi.
“Dany najua kwamba kwa sasa upo katika wakati mgumu sana, ila ninakuomba uvumilie kwa kila kazi inayo kuja mbele yako”
“Muheshimiwa raisi ninalitambua hilo, ninakuomba umlinde mke wangu”
“Nitahakikisha hakuna baya linalo mpata na ataishi hapa ikulu kwa kipindi chote ambacho utahitaji aweze kuishi hapa”
“Nashukuru kwa kusikia hivyo”
“Basi kwa sasa mke wako anaweza kutueleza juu ya mtoto wa huyo kiongozi wa boko haramu na kuanzi hapo tunaweza kuianza kazi”
“Sawa muheshimiwa raisi”
“Siku njema”
Nikakata simu na kumrudishia meja.
“Tutawahitaji katika chumba cha maelezo baada ya nusu saa”
 
“Sawa meja”
Nikabaki na Hawa ndani ya chumba hichi, nikapiga hatua hadi mlangoni, nikaufunga mlango kwa ndani na kurudi kitandani. Nikamuinamia Hawa na kuanza kumnyonya midomo yake taratibu Hawa akaanz akuipitisha mikono yake nyuma ya mgongo wangu jambo lililo zidi kutufanya tuzidi kuzama kwenye dimbwi zito la mapenzi. Taratibu nikamchomoa Hawa sindano iliyo chomwa kwenye mkono wake inayo ingiza maji kwenye mishipa yake.
Nikavua tisheti yangu na kubaki kifua wazi.
 
“Dany”   
“Mmm!!”
“Naomba”
Hawa alizungumza kwa sauti iliyo jaa mahaba mengi ndani yake,  Nilipo hakikisha kwamba yupo vizuri taratibu nikaanza kula . Kila mmoja akajitahidi kuhakikisha kwamba anamridhisha mwenzake kwa kadri awezavyo yeye mwenyewe. Mechi yetu ikamalizika ndani ya nusu saa, na sote tukajikuta tukiwa tumeridhika kwa tulicho kifanya. Taratibu nishuka kitandani, nikamnyanya Hawa kutoka kitandani, nikambeba hadi bafuni ambapo ni humu humu ndani ya hichi chumba.
 
“Dany natambua kwamba hii kazi ambayo unayo iendea ni hatari sana, ila inabidi uwe makini mume wangu kwa maana bado ninakuhitaji na bado ninakutegemea kwenye maisha yangu. Kwa sasa wewe ndio baba, wewe ndio mama na wewe ndio ndugu”
“Usijali Hawa nitahakikisha kwmaba kila jambo linakwenda sawa kama tulivyo panga sawa mama”
“Sawa mume wangu, ila ninakuomba sana tena sana uwe makini, ukishindwa hii kazi ninakuoba urudi tu, tutatafuta hata sehemu ya kwenda kuishi wawili, hakutakuwa na haya ya wewe kuendelea na haya mambo, nahitaji uwe baba mzuri atakaye ilinda familia yake kwa garama yoyote itakayo jitokeza kwenye maisha yake”
 
“Nitakuwa baba mwema, nitahakikisha hizi kazi mbili ninazimaliza, na nikimaliza hapo nitaachana na kila jambo ambalo linauhusiana na kulipiza kisasi ama usalama”
“Nitashukuru mume wangu”
Taratibu Hawa akanikumbatia huku machozi yakimwagika, taratibu nikakilaza kichwa chake kifuani mwangu huku nikimbembeleza taratibu. Taratibu Hawa akaniachia huku akifuta machozi yake usoni mwake, akaizungusha koki ya bomba iliyopo pembeni, taratibu maji yakaanza kutumwagika mwilini mwetu. Tukaanza kuogeshana huku tukicheza baadhi ya michezo ikiwemo kutekenyana katika mbavu zetu.
 
“Hapo awali sikuweza kufahamu kwamba mapenzi yana raha. Baada ya kurudi Somali juzi, nikliona maisha yangu kwangu ndio basi tena, nilihisi kwamba sinto kuona tena, na baba yangu alinihitaji kukusahau ila haikuwa rahisi kama alivyo dhani. Nililia sana, nilijaribu kujiua kwa mara kadhaa, ila niliweza kuzuiliwa, ila jana nilivyo weza kusikia uwepo wako, sikuweza kuamini sana hadi pale nilipo kuona. Dany moyo wako ninakuomba usimpe mwanaume yoyote, tafadhali ishi na mimi, tafadhali linda pemzi langu, chochote kitakacho tokea kwenye maisha yetu nakuomba ukumbuke una mwanamke anaye jiheshimu na kukupenda katika maisha yake yote”
 
“Shukrani Hawa, nitakupenda na kukujali katika maisha yangu, na kama jana ungejiua na baba yako wala nisinge weza kuifikisha siku ya leo na mimi ningekuwa nimesha jiua”
“Ila Mungu hakupanga iwe hivyo”
“Kweli”
“Tumalize nahisi watakuwa wanatusubiria sisi”
Tukamalizia kuogo na kutoka bafuni, Hawa akavaa nguo zake wanazo vaa wagonjwa huku na mimi nikivaa kombati zangu za jeshi. Nikaufungua mlango, nikakutana na meja akiwa amesimama na inaonekana ni kwa muda mrefu alikuwa amesimama akisubiria tumalize kufanya tunacho kifanya ndani ya chumba hichi.
“Tunaomba dakika tano meja”
“Sawa”
 
Nikaurudishia mlango na kumsogelea Hawa, nikazishika nywele zake ndefu zinazo karibia kufika mgongoni, taratibu nikaziweka vizuri huku tukitazamana. Nikambusu mdomoni mwake, kisha na kumshika mkono wake wa kulia.
“Upo tayari kwa kutoka?”
“Ndio honey”
Tukatoka kayika chumba hichi, tukaongozana na meja hadi kwenye chumba kikubwa, tukakuta viongozi baadhi wa jeshi, pamoja na Tv kubwa.
“Tutawasiliana na raisi muda si mrefu”
“Sawa”
Tukaka kwenye viti viwili ambavyo tayari vilisha andaliwa kwa ajili yetu. Tv hii kubwa ikawasha na tukamuona raisi akiwa katika ofisi yake nchini Marekani. Akatusalimia wote kwa pamoja na sote tukaitikia.
 
“Nisiwapotezee muda mwingi sana katika hili tunalo kwenda kulijadili hapa, ila kitu kikubwa kwamba, jana tumefanikiwa kuangusha kundi moja la Al-Shabab hapo nchini Somalia, na kiongozi wao amaeweza kuuwawa.”
“Opareshini inayo fwata kwa sasa ni kuliangamiza kundi la Boko Haramiu, ambapo wiki iliyo pita tu, liliweza kuvamia shule ya wanafunzi wa kike nchini Nigeria na kuweza kuwaua mia moja na sita huku wanafunzi mia tatu hadi sasa havi serikali ya Nigeria wala sisi hatujui ni wapi wabini hao walipo”
 
“Opareshni hii, nimemkabidhi Dany, na yeye ndio atakuwa mpelelezi katika kuweza kufahamu ni wapi kundi hilo lililo na ni wapi wanafunzi hao wameshikiliwa, kwa maana kwa sasa hatujadilia maswala ya Marekani peke yake, ila tunajadili maswala ya dunia nzima kwa ujumla. Mrs Dany amekiri na kusema kwamba anaye mtu wa karibu sana na kundi la Al-Shabab, ambaye anaweza kutuongoza sisi kufahamu ni wapi lilipo kundi hilo. Sasa Mrs Dany ninakuomba uweze kuteleza ni wapi tunaweza kumpata huyo rafiki yako”
 
Sote tukamtazama Hawa, aliye nitazama na mimi kwa sekunde kadhaa kisha akamtazama raisi tunaye muona kupitia hii Tv kubwa.
“Rafiki yangu anaitwa Yemi Okocha, ni mwana mitindo mkubwa sana nchini hapo Nigeria, na kazi zake pia baadhia nazifanya nchini Marekani pamoja na South Afrika. Yemi Okocha sio jina lake la kuzaliwa, ila jina lake halisi anaitwa Tayana Mohamed Alade. Baba yake ndio kiongozi wa Boko Haramu, alikuwa ni mwajeshi aliye hasi inchi yake na kutengeneza kundi lake hilo kubwa, linazo zidi kupata umaarufu siku hadi siku.”
 
Mtaalamu wa maswala ya mitandao, kwa haraka aliweza kutuletea picha ya Yemi Okocha, kwenye kila Laptop iliyopo katika meza hii. Ni binti mzuri sana, mredu mwenye umbo zuri ana kila sifa ya kuitwa msichana mzuri.
“Makao makuu ya Yemi Okocha ni Victoria Island Lagos na jina la kampuni yake ni Y.O Entertiment. Hayo mimi ndio ninayo yafahamu kuhisiana na Yemi Okocha, ninamaini kwamba yatakuwa ni muongozo mzuri sana kwa Dany kuanza kuifanya kazi yake”
“Tunashukuru kwa msaada wako mkubwa Mrs Dany. Naamini mumesikia wote, sasa hapo ninacho hitaji ni kuweza kufahamu mchango wenu ni jinsi gani Dany anaweza kwenda na kuanza kuifanya hii kazi”
 
“Muheshimiwa raisi nianze kwa kuzungumza mimi mwenyewe, mpango mzima wa kwenda kuifanya hii kazi ningeomba uniachie mimi, japo ninaamini kwamba itachukua muda mrefu kiasi ila itabidi nifanye hi
vyo ili kazi yetu iweze kukamilika. Ninacho kiomba katika hili, ninaomba pesa ya kutosha na nitakwenda kama raia wa kawaida kabisa kwa maana katika hili hakuna haja ya kutumia nguvu ya jeshi kwani inaweza kwenda kuinua vita kubwa. Tukiweza kupata uhakika kwamba ni wapi kundi la Boko Haramu lipo basi hapo hata nguvu ya jeshi itahitajika”
“Sawa nimekuelewa sana Dany, je kuna mtu ana jambo la kuchangia katika hii oparesheni”
Watu takatazamana na hakuna aliye zungumza kitu chochote, ikimaanisha kwamba hakuna ambaye anahitaji kuchangia chochote. 
 
“Basi meja ninakuachia jukumu zima la kuhudumia hati za usafiri kwa Dany, pamoja na pesa atakayo hitaji basi aweze kupatiwa”
“Sawa muheshimiwa raisi”
“Kikao kimekwisha”
Tv ikazimwa, taratibu tukanyanyuka, nikamshika Hawa mkono na kutoka katika chumba hichi.
“Meja naomba unipatie simu niwasiliane na raisi moja kwa moja?”
“Kuna tatizo?”
“Hili ni jambo binafsi”
“Sawa”
Meja akanipatia simu yake ambayo tayari alisha mpigia raisin a simu ipo hawani.
“Ndio meja”   
“Hapana muheshimiwa raisi ni Dany hapa”
“Ndio Dany”
“Hatujazungumzia kuhusiana safari ya mke wangu?”
“Kuna private Jet ipo jiani inakuja kumchukua mke wangu, nilihitaji kukuambia hilo baada ikiwa imesha fika, naamini baada ya msaa manne itakuwa imesha fika hapo”
 
“Shukrani muheshimiwa raisi kwa kunijali katika hili”
“Karibu na nijukumu langu mimi kuweza kufanya hivyo”
“Basi ikifika nitakujulisha muheshimiwa raisi”
“Sawa”
Nikakata simu na kumkabidhi meja simu yake.
“Dany pesa, yote itaingizwa kwenye akaunti yako ambayo kwa sasa ipo katika hatua za mwisho kufunguliwa. Hati pamoja na vitu vyote vinatengenezwa, ila itabidi kwa sasa utumie jina tofauti na Dany”
“Jina gani?”
“Utatumia Peter Lukas Otieno, uraia wako utaonekana kwamba wewe ni Mkenya, hakikisha kwamba hilo unaliweka kichwani mwako”
“Nimekuelewa meja”
“Mrs Dany, utaongozana na nesi hapo, utaeleka chumba cha mavazi, utaandaliwa nguo zako za safari ndani ya muda mfupi ndege binafsi ya raisi itatua katika kiwanja chetu na safari ya Marekani itaanza”
“Sawa meja”
“Dany naomba unifwate”
Nikambusu Hawa kwenye paji la uso kisha tukaachana na mimi nikaongozana na meja hadi katika ofisi yake. Akanikaribisha kwenye sofa nzuri zilizopo kwenye hii ofisi, sote tukaka.
 
“Unahitaji kinywaji?”
“Hapana, sijapata chai hadi sasa hivi”
“Ohoo basi mukumbuke kupata kifugua kinywa hata kabla ya mke wako hajaondoka.”
“Sawa meja”
“Dany kitu ambacho ninakuomba, ninatambua kwamba unampenda sana mke wako, natambu hilo kwa muda mchache ambao tumekaa hapa”
“Ni kweli?”
“Kitu kikubwa ninacho kuomba katika hii oparesheni hakikisha unafanya jambo lolote ili hoyo msichana awe mikononi mwako, hata ikiwezekana tumia njia ya usaliti”
“Uma naanisha nini meja?”
“Hata kwa kutembea naye kimapenzi fanya hivyo, japo natambua utahatarisha ndoa yako ila hakutakuwa na jinsi nyingine ya kufanya ziaid ya kuwa na mahusiano na msichana huyo kwa maana una vigezo vyote vya kumvutia mwanamke yoyote, hata awe mke wa mtu ni lazima atavutiwa na wewe tu.”
Maneno ya meja yakanifanya nikae kimya huku nikishusha pumzi nyingi na maneno ya Hawa baadhi tuliyo yazungumza bafuni kuhusiana na kulilinda penzi letu yakaanza kunirudia kichwnai mwangu tarataibu.


AISIIIII……….U KILL ME 131

   
“Dany, Dany”       
Sauti ya meja ikanistua kutoka katika dibwi zito la mawazo ya maneno ambayo tuliyapanga mimi na Hawa.
 
“Naam”
“Natambua ya kwamba ni ngumu sana kumsaliti mke wako ambaye unampenda.Unajua kipindi nilipokuwa na umri kama wako, nilikuwa na mwanamke niliye mpenda sana japo kwa sasa ni marehemu, ila hadi leo ninaamini kwamba kifo chake nimekisababisha mimi ila sikuwa na jinsi”
Meja alizungumza kwa sauti ya chini huku akinitazama usoni mwangu.
“Basi nilimpenda sana Elistrida, tangu tulipokuwa shule ya msingi tulianzisha mahusiano hadi tukafikia umri wa kuona. Mipango ya harusi ilifanyika, mwezi mmoja kabla ya harusi yetu niliweza kupewa kazi ya upelelezi kwenda nchini Pakistani, nilipewa jukumu la kuweza kuchunguza ni wapi lilipo kundi la Alquida.”
 
Nikaanza kumuona meja machozi yakianza kumlenga lenga usoni mwake, ila nikazidi kujikausha kimya ili kuendelea kusikiliza kwa kile anacho nisimulia kwa muda huu.
“Nilipata mwanamke mmoja wa kipakistani, ambaye niliambiwa nihakikishe kwamba ninamueka mikononi mwangu hususani kimapenzi, kutokana kipindi kile nilikuwa kijana mzuri, bado uso hajajikunja na uzee huu, basi niliweza kufanya kama nilivyo fanya. Yule msichana alinipenda sana ndani ya muda mchache sana, aliweza kunipatia kila aina ya taarifa niliyo kuwa nina ihitaji. Nilipo fanikiwa kumaliza kazi yangu, basi niliondoka nchini Pakistani na kurudi Marekani pasipo msichana yule kufahamu.”
 
“Nikiwa sielewi ni kitu gani kinacho endelea nyuma yangu, siku ya harusi ikawadia, huku baadhi ya wakuu wangu wa kijeshi waliweza kufika kanisani. Tukiwa katikati ya ibada pale kanisani, Tv zote kubwa ndani ya kanisa, zikaanza kuonyesha video ya ngono ambayo nilikuwa na yule msichana, kumbe yule binti kila kitu tulicho kuwa tunakifanya alikirekodi pasipo mimi kufahamu”
Meja machozi yakaanza kumchuruzika kwenye mashavu yake, japo ni mzee wa miaka kama stini ila ameshindwa kabisa kuyazuia machozi yake mbele yangu.
 
“Mke wangu baada ya kuona vile, akachanganyikiwa kabisa, akaanza kukimbia kuelekea nje ya kanisa, nguvu ziliniishia, ila baadhi ya wanajeshi walijaribu kumshika, katika kurupushani za kumshika, akachomoa bastola ya kijana mmoja na kwa haraka sana aliweza kujipiga risasi ya mdomo na ikatokea nyuma ya kich……”
Meya akashindwa kumalizia hadithi yake na machozi yakazidi kumwagika usoni mwake, taratibu akanayanyuka kwenye sofa alilo kalia na kutemeba hadi katika kiti kilichopo hapa ofisini kwake. Kwa ishara akaniomba nitoke ndnai ya ofisi yake. Taratibu nikanyanyuka na kumtazama usoni mwake, akaendelea kunisisitizia kwa ishara nitoke ofisini kwake. Taratibu nikachukua kitambaa kilichopo juu ya hii meza, nikakikunja vizuri na kuwa kitambaa ambacho anaweza kujifutia machozi, kisha nikamuwekea juu ya meza yake na kutoka ofisini hapa.
 
“Nesi”       
“Ndio”
“Mke wangu yupo wapi?”
“Yupo katika chumba cha mavazi”
“Unaweza kunipeleka?”
“Hakuna shaka katika hilo”
“Sawa”
Nikaongozana na nesi hadi katika chumba cha mavazi, nikamkuta Hawa akipimwa pimwa vipimo vya nguo. Nesi akatoka na kuniacha nikimtazama Hawa na wapimaji hawa ambao nao ni wanajeshi wa kike ila wana fani ya ufundi.
“Dany nimepungua eheee”
Hawa alizungumza huku akinifwata usoni mwake akiwa amejawa na tabasamu pana.
 
“Sio sana”   
“Ila ni tofauti na mwanzo?”
“Yaa ila kwa hekaheka ambazo tumezipata kupungua ni lazima”
“Kweli vipi mbona unaonekana kama huna raha mume wangu?”
“Hapana, mke wangu, wanakushonea kitu gani?”
“Kuna suti mmoja wamenionyesha picha nikaipenda sana”
“Waoo sasa wanaweza kuimaliza kwa leo?”
“Sio leo tu yaani wataimaliza ndani ya dakika kumi na tano, yaani hawa wadada ni wataalamu sana”
“Duuu kazi kweli kweli”
Nilijaribu kujifurahisha ila kusema kweli woga umesha anza kuniingia katika moyo wangu, kwani historia ya meja, imenifanya nipoteze hata hamu ya kuifanya kazi iliyopo mbele yangu.
 
“Dany ninakujua vizuri sana mume wangu, ninakuomba uniambie ni kitu gani ambacho kinakusumbua akilini mwako?”
Hawa alizungumza huku akinitazama usoni mwangu kwa macho makali. Nikaka kimya kwa sekunde kadhaa, nikawatazama wadada ambao tayari wamesha anza kuishona suti ya Hawa wakishirikiana. Nikamshika Hawa mkono wa kulia, tukasogea hadi kwenye viti vilivyopo mbali kidogo na hawa wadada japo ni ndani ya hichi chumba.
“Niambie mume wangu una tatizo gani?”
“Baby ninaogopa kuifanya hii kazi”
Hawa taartibu akashusha pumzi huku akinitazama kwa sura ya masikitiko, taratibu akanishika mashavu yangu kwa viganja cya mikono yake. 
 
“Dany natambua unaogopa kwa maana sehemu unayo kwenda ni mpya na hakuna mtu hata mmoja ambaye unamjua au aliwahi kukufanyia ubaya. Ila kumbuka kwamba hii ni vita mume wangu. Dunia nzima, watoto wadogo, wanamama, wasichana ambao wanaishi katika mateso ya kukimbia vita kila siku wanakutazama wewe, wanakutegemea wewe. Hii ni nafasi ya pekee ambayo hata kwa Mungu ninaamini atakuandikia dhwawabu. Tafadhali Dany usiniangushe chini, nipo nyuma yako hakikisha kwamba unanifanya nijisifie mbele za wanawake na hata dunia kwa ujumla kwamba mume wangu ni mtu imara na mtu makini sana”
 
Hawa alizungumza kwa sauti ya upole iliyo jaa ushawishi na mahaba mazito ambayo taratibu nikajikuta nikiishiwa na wasiwasi ambao ulikuwa umeanza kunitawala moyoni mwangu.
“Ila mke wangu sielewi hii kazi ninaanza anzaje kuifanya hembu ninaomba unipe japo mwangaza kidogo, ili niweze kufahamu kwamba binti huyo anapendelea kitu gani?”
“Ahaa, Yemi anapenda sana kuogelea, nakumbuka kipindi tupo chuo, alikuwa hapitishi hata siku mbili kabla ya kwenda kuogelea, pia Yemi anapenda sana chocolate, hivyo ni vitu vikubwa sana anavyo vipenda”
 
“Chocolate!!?”
“Yaa mbona unashangaa mume wangu?”
“Hicho ni kitu cha kaiwada sana”
“Mume wangu hujatujua sisi wanawake hususani kwa sisi ambao tunatoka katika familia za kitajiri, huwa hatapendi vitu vikubwa kwa maana kila kitu tumekikuta kwenye familia zatu na si washamba sana wa kushadadia vitu vikubwa kama gari na mambo mengine kama ilivyo kwa kuwa kwa wasichana hawa wa kawaida”
“Sawa mke wangu, sasa daaaa.”
“Dany hii kazi ndio itakufanya wewe uwe juu zaidi ya hapa ulipo. Ifanye kwa moyo mmoja, hata siku mtoto wetu aje kujisifu kuwa na baba kama wewe”
 
“Nimekuelewa mke wangu nitafanya, Mungu aniongoze katika hili”
“Namini hakuna utakacho shindwa”
Maneno ya Hawa yakazidi kunifariji na kunipa moyo wa kuifanya kazi iliyopo mbele yangu. Katika muda huu tulio kaa hapa, washonaji hawa wakawa wamemaliza kushona suti ya Hawa. Wakamkabidhi, akaijaribisha na kwa jinsi Hawa alivyo penda suti yake iwe ndivyo ilivyo kuwa.
“Umependa mke wangu”
“Yaa siivui hii suti hadi Marekani”
“Hahahaa, usifanye hivyo mke wangu”
“Sikutanii honey, hapa ndio imetoka”
Malango wa chumba hichi ukafunguliwa, akaingia meja akiwa katika hali ya furaha hadi nikabaki nikiwa nimeduwaa.
“Mrs Dany umependeza sana”
“Nashukuru meja”
“Sasa ndege imesha fika, sijui upo tayari kwa safari tuelekee uwanjani?”
Hawa akaniangalia usoni mwangu na akabaki akiwa na kigugumizi kilicho nifanya nijibu mimi.
 
“Ahaa meja naomba nipate kifungua kinywa na mke wangu kisha baada ya hapo tutaelekea uwanjani”
“Sawa tuongozane katika bwalo la chakula”
Tukaelekea katika jengo linalo tumika kwa wanajeshi kuweza kupata chakula. Tukahudumiwa na wahudumu wa hapa.
“Kusema kweli Dany na mke wako mumeendana sana, sipati picha mtoto wenu atafananiaje?”
“Atafanana na baba yake?”
“Mmmm mimi nnataka mwanagu afanane na mke wangu?”
“Wapi atafanan na wewe kwa maana wewe ndio baba”
“Sasa akiwa wa kike unataka nifanane naye pia?”
“Tena ukifanana naye atakuwa bonge moja la mrembo kwa maana mmmmmm, mume wangu wewe mzuri. Ila ninakuomba kwamba huko unapo kwenda tafadhali ninaomba unilindie penzi langu, sinto taka kusikia wala kujua kwamba umeingia kwenye mahusiano na msichana yoyote mume  wangu sawa”
 
Tukatazamana na meja kwa macho ya kuiba, jambo ambalo Hawa hakulistulia kabisa. Nikatabasamu kidogo huku nikijiweka vizuri shati langu.
“Sasa kwa mfano ukajua mume wako ametoka kimahusiano na mwanamke mwengine inakuwaje?”
“Ahaa bora oparehsni ife kwa kweli, wanawake wa sasa wana magonjwa mengi, ninampenda mume wangu, nahitaji tujenge familia yenye afanya”
“Ila hujanijibu kwamba ukijua  kwamba imekuwa hivyo utafanyaje?”
“Huyo mwanamke kwanza nitashuhulika naye kwa kweli, ni bora nirudi katika hali yangu ya ugaidi kwa muda wa kumshuhulikia huyo mwanake kisha sasa hapo ndipo hali ya kawaida itaendelea”
Nikamuona meja akishusha pumzi taratibu taratibu huku akinitazama kwa umakini sana.
 
“Ahaa mke wangu hilo jambo haliwezi kujitokeza nakupenda sana”
“Natambua hilo mume wangu na ninakuamini katika hilo”
“Nashukuru kwa kuniamni”
Tukamaliza kupata kifungua kinywa, tukaingia kwenye gari la jeshi na moja kwa moja likatupeleka hadi uwanja wa ndege. Tukakuta mizigo ya mabegi ya Hawa, iliyo jazwa nguo ikiwa tayari imesha fikishwa kwenye uwanja wa ndege. Tukashuka kwenye gari na kuanza kutembea hadi ilipo ndege hii ya kifahari inayo milikiwa na raisi wa Marekanani. Nikamsaidia Hawa kuingiza mabegi ndani ya ndege hii inayo beba abiria wasiozidi wanne.
“Mke wangu unakwenda Marekani, ninakuomba uwe makini sana, ninakuomba uhakikishe kwamba unanitunzia penzi langu, sihitaji siku itokee nijue kwamba una mwanaume mwengine ndani ya ikulu, utanifanya nibadilike, utafanya zoezi hili lote libadilike na kuwa baya sawa mke wangu”
 
Nilizungumza huku nikiwa nimekumbatia Hawa, ndani ya hii ndege.
“Nimekuelewa mume wangu, siwezi kufanya hivyo, naytambua thamani yako. Natambua umuhimu wako kwangu, nakuahidi kamwe sinto weza kufanya ujinga wa aina yoyote wa kukuumiza wewe roho”
“Ninashukuru mke wangu”
. Taratibu tukaachiana huku sote tukilengwa lengwa na machozi.
“Nakupenda sana mume wangu”
“Hata mimi pia ninakupenda, ninakuomba ukae sasa uanze safari”
 
Taratibu nikamkalisha Hawa kwenye siti, nikamfunga mkanda wa siti, taratibu nikambusu kwenye paji la uso wake, kisha nikambusu kwenye midomo yake na taratibu nikaanza kushuka pasipo kuangalia nyuma kwa maana Hawa, alisha anza kuangua kilio.
Nikapiga hatua hadi alipo Meja, taratibu mlango wa ndege hii ukafunga, mlio wa ndege ukaanza kutawala kwenye masikio yetu, taratibu ndege hii ikaanza kuondoka eneo hili, hatukuhitaji kuondoka hadi tulipo ishuhudia inaicha ardhi ya Somalia nasi ndio tukajikuta tukitazamana.
“Mke wako yale aliyo yazungumza ana yamaanisha”
“Ni kweli meja, na Hawa akizungumza ujue amezungumza inabidi kuwa makini naye sana katika hili la sivyo tutajikuta tunashindwa kufanya kitu chochote kwenye hii oparesheni”
 
“Kweli Dany”
Tukaingia kwenye gari na safari ya kurudi kwenye majengo yetu ukaanza. Simu ya meja ikaanza kuita, akaitoa mfukoni mwake na kuipokea.
“Ndio”   
“Sawa tupo njiani tunakuja”
Akakairudisha mfukoni mwake na kunigeukia.
“Hati zako za kusafiria zipo tayari na utaondoka na ndege ya saa mbili usiku”
“Sawa meja, na jina nitakalo litumia ni Peter”
“Yaa, uraia wako ni Kenya”
“Sawa meja”
Tukafika ofisini kwa meja, nikakabidhi kila kitu pamoja na kadi ya benki ambayo inaonyesha jina langu pamoja na picha yangu.
“Kwenye akaunti yako ya beki kuna dola laki tano, nina amini kwa kipindi chote utakacho kaa Nigeria zitakusaidia na endapo zitakuishia, basi utawasiliana nasi”
 
“Sawa meja”
“Nguo zako zipo katika chumba kingine, huko huwezi kwenda na hizi gwanda, wasije wakakustukia bure wakakuua mapema”
“Kweli meja”
“Basi unaweza kupumzika, hadi saa moja moja tutaonana, na nitakusindikiza uwanja wa ndege”
“Nitashukuru meja”
Nikatoka ofisini kwa meja na kumuacha aendelee na majukumu mengine. Nikaingia katika chumba cha mavazi ya kiume ambacho kipo karibu kabisa na chumba cha mavazi ya kike. Nikachagua nguo chache za kuvaa niendapo, nilipo hakikisha kwamba nimepata nguo nzuri, nikaziweka katika begi dogo la mgongoni huku nikiwa nimezikunja vizuri. Nikahifadhi hati yangu ya kusafiria ila kadi yangu ya benki nikabaki nayo mfukoni.
 
Nikaanza kuzunguka maeneo ya kambi hii ya jeshi, ambayo kusema kweli imejengwa kwa ustadi wa hali ya juu na ina eneo ambalo ni kubwa sana, nikaanza kutazama jinsi wanajeshi wa Kimarekani wanavyo fanya mazoezi yao hususani ya kijeshi, nikafika kwenye moja ya kiwanja nikakuta wanafanya mazoezi ya jinsi ya kumlinda raisi pale anapo vamiwa kwenye msafara, kusema kweli nikajukuta nikufurahi sana, japo mimi mwenyewe nilisha wahi kuyajifunza nilipo kuwa nipo NSS, ila mafunzo yao yana ubora kulilo niliyo fundishwa mimi miaka kadhaa iliyo pita.
 
    Saa kumi na mbili jioni nikarudi kwenye chumba cha mavazi, nikaingia kwenye bafu lililopo hapa chumbani, nikaoga na kubadilisha nguo zangu. Nikavaa suruali ya jinsi yenye gengi yeusi pamoja na tisheti nyeusi iliyo nibana vizuri mwili wangu, nikava buti yeusi za kisasa, nikabeba begi langu la ranyi nyeusi, mgongoni kisha nikatoka katika chumba hichi. Nikaingia ofisini kwa meja, nikamkuta akipanga panga mafaili yake vizuri.
“Hapo upo vizuri, tunaweza kuondoka sasa”
“Sawa meja”
Tukaeleka kwenye gari binafsi la meja, tukapitia kwene moja ya nyumba anayo ishi humu ndani ya kambi, akabadilisha nguo zake na safari ikaendelea. Tukafika uwanja wa ndege wa nchini Somalia ulipo hapa Mogadishu. Kabla ya kushuka kwenye gari, meja akanipatia kibunda cha dola mia mia zilizo fungwa vizuri.
 
“Ni dola elfu kumi, utatumia kwa kuanzi maisha”
“Nashukuru sana meja”
“Nikutakie safari njema”
“Shukrani”
Nikashuka kwenye gari na moja kwa moja nikaanza kuelekea kwneye gari huku nikiwa makini sana. Nikapanga foleni kwenye mstari wa abiria wanao suburia kukaguliwa. Mbele yangu kuna dada wa kizungu ameshika kioo kikubwa kiasi akijipamba nyusi zake, nikabahataika kupata upenyo mdogo wa kuangalia mtu aliye nyuma yangu, nikajikuta nikistuka baada ya kuona jamaa wawili wa kiarabu wenye ndevu nyingi wakiwa nao wamesimama kwenye hii foleni. Nikavuta kumbukumbu kwamba ni wapi nilipo waona jamaa hawa wawili. Kumbukumbu zangu zikaangukia katika kambi ya Al-Shabab, na mmoja kati ya hawa jamaa alikuwa ni mlinzi wa baba Hawa, sijafahamu ni wapi wanapo elekea ila mstari ambao nipo mimi sote tunapanda ndege moja, hapa ndipo nikaanza kupata wasiwasi mkubwa sana juu ya hawa jamaa kama hawapo hapa kwa ajili ya kutoroka basi wapo hapa kwa ajili yangu kwani mimi ndio muharibu mkubwa wa kambi yao.

==>>ITAENDELEA KESHO


from MPEKUZI

Comments