MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA
Nilizungumza huku nikifunga kiwambo cha kuzuia sauti kwenye bastola yangu, nikajisogeza kwenye mti mwingine taratibu pasipo wao kuweza kuniona. Kitendo cha mwanajeshi mmoja kunyanyua simu yake ya upepo na kuhitaji kuwasiliana na wezake ikawa ni kosa kubwa kwangu kwani sikuwa na jinsi ya kufanya zaidi ya kumuua mwajeshi huyu kwa kumpiga risasi ya kichwa jambo lililo mfanya mwenzake kubaki akiwa ameduwaa asijue hata cha kufanya kwani mkononi mwake hana hata silaha ya kujitetea.
ENDELEA
Nikajitokeza kwenye mti huu huku nikiwa nimeishika bastola yangu nikimuelekezea mwanajeshi huyu. Kwa ishara nikamuamrisha anyooshe mikono yake juu, akafanya hivyo tena kwa haraka sana, huku mwili mzima ukitetemeka.
“Weka vitu vyote mulivyo toa ndani ya hili begi”
Nilijaribu kuzungumza kisomali, japo ninachapia baadhi ya maneno ila nina imani mwajeshi huyu ameelewa nilicho muambia. Kwa haraka akaanza kuingiza kitu kimoja baada ya kingine nilipo hakikisha kwamba amemaliza kuviweka vitu hivi, nikamuomba begi langu. Akanikabidhi, taratibu nikalivaa mgongoni mwangu. Nimamtazama jinsi mikono inavyo lowanisha shuruali yake, roho ya huruma ikaanza kunitawala, ila nikimuacha hai huyu naye inaweza kuwa tatizo. Nikampiga risasi moja ya kichwa na kumfanya aanguke chini na kupoteza maisha yake hapo hapo.
“Dany kwa nini na huyo umemua?”
“Sikuwa na jinsi muheshimiwa raisi, ninafanya kile ninacho kiona ni bora kwa hii opareheni”
“Sawa”
Nikaitazama PDA yangu na kuanza kuitafuta ramani ya kuelekea katika kambi ya Al-Shabab, kutoka hapa nilipo kuna umbali wa kilomita tano, ambazo nilazima nitembea ndani yam situ huu hadi kufika hapo. Nikaianza safari huku nikiwa makini sana kuhakikisha kwamba sikutani na wanajeshi wa serikali wanao fanya opareheni kwenye huu msitu ambao hata sifahamu jina lake. Saa yangu ya mkononi ikanionyesha ni saa kumi na moja kasoro alfajiri, nikazidi kusonga mbele ili kwamba nitumie muda mwingi sana katika kutembe ili hata kama asubuhi itanikuta kwenye huu msitu basi ninaami nitahakikisha kwamba ninakaa ndani ya huu msitu hadi usiku ili niendelee na uvamizi wangu katika kambi ya Al-Shabab, kwani kwenda mchana ni hatari kwa maisha yangu.
Hadi kuna pambazuka bado nipo ndani ya huu msitu ulio jaa vilima pamoja na mawe mengi, kwa mara kadhaa nilipumzika ili hata jioni ikifika nisiwe nimechoka sana. Katika siku ninayo ona masaa yanakwenda taratibu ni hii ya leo sikukuata tamaa zaidi ya kuzidi kusonga mbele.
“Dany umebakisha muda gani kuweza kufika katika ngome ya Al-Shabab?”
“Kama nusu kilomita muheshimiwa. Nitahitaji kufika usiku kwa maana mchana huu ni hatari kwangu”
“Sawa jukumu lote lipo juu yako, vikosi vya anga vinasubiria amri yako”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Pole pole ndio mwendo, kweli usemi huu kwa siku ya leo kwangu umeweza kukamilika, kwani hadi inafika usiku saa mbili, nikawa nimefanikiwa kufika jangwani ilipo kambi ya Al-Shabab, nikaanza kutemeba sasa kwa tahadari katika jangwa hili kwa maana katika ngome ya Al-Shabab kuna minara ya wanajeshi wanao kaa kwa juu na wanamuona mtu wa mbali sana anapo karibi kufika katika ngome yao. Nikafika kwenye moja ya kichuguu cha mchanga, nikapanda juu na kulala taratibu. Nikaitoa bunduki yangu moja kwenye begi na kuanza kuiunganisha kipande kimoja baada ya kingine. Ilipo kamilika, nikaifunga lensi ambayo inaniwezesha kumuona mtu wa mbali kwa ukaribu mkubwa sana. Uzuri lensi niliyo ifunga inatumika kuona mtu hata akiwa gizani, haina tofauti sana na miwani zinzo tumika usiku.
Nikafanikiwa kuona mmnara mmoja kwa sehemu ninayo tokea, huku taa kubwa likiwa lina mulika eneo zima huku likizunguka zunguka.
“Muheshimiwa raisi oparesheni imeanza”
“Kazi njema Dany”
“Asante”
Nilipo hakikisha kwamba nimemuweka mwajeshi mmoja wa Al-Shabab katika tageti yangu, taratibu nikafunga kiwambo cha kuzia sauti, kisha taratibu nikavuta triga ya bunduki yangu na ninakiruhusu riasi kutoka kwa kasi, wala haikumaliza sekunde mbili mwajeshi huyu aliye kaa juu ya mnara kwenye kibanda kidogo akaanguka chini. Nikatazama eneo lote la karibu sikuona mwanajeshi yoyote, nikaishika bunduki yangu hii ambayo ni nzito kiasi, nikaanza kukimbia nayo huku nikiwa makini sana kitazama mbele. Nikafanikiwa kufika kwenye ukuta wa ngome wa hii kambi, nikatoa kamba yangu ndefu kwenye begi ikiwa na nanga ndogo yenye ncha zilizo kikunja tatu.
Nikairusha juu ya ukuta kwa kutumia nguvu zangu zote, nikajaribu kuivuta, haikuweza kushuka chini, nikaiuvaa mkanda wa bunduki yagu mgongoni, huku beg langu nalo pia likiwa mgongoni, nikaanza kupanda ukuta huu mrefu kwa kasi ya ajabu huku nikiwa makini sana. Cha kumshukuru Mungu nikafanikiwa kufika juu kabisa ya huu ukuta. Nikachuchumaa kwa umakini sana huku nikitazama kwa ndani, wanajeshi wapo doria na nina imani hakuna hata mmoja ambaye anaelewa juu ya uwepo wangu humu ndani. Nikaanza kuivuta kamba yangu kwa haraka huku nikiikunja, ili kufuta ushahidi hata kama ikitokea wanajeshi wanao fanya doria nje ya hii ngome wasiikute.
“Nipo ndani muheshimiwa raisi, waambie timu ya wanajeshi mia moja wawe karibu kabisa”
“Sawa ndani ya dakika kumi na tano watakuwa maeneo ya karibu.”
“Sawa mimi ninaelekea moja kwa moja kwenye nyumba anayo ishi mkuu wao”
“Sawa”
Uzuri katika huu ukuta kwa huku ndani kuna ngazi za kushukia, taratibu nikaanza kushuka katika hizi ngazi, nikafanikiwa kufika chini pasipo mtu yoyote kueweza kuniona. Nikaanza kueleka katika nyumba anayo ishi baba Hawa, na uzuri ni kwamba eneo nililo ingia lipo karibu kabisa na ilipo nyumba ya baba Hawa.
Nikafika katika gorofa analo ishi baba Hawa, nikavua begi langu nikalificha kwenye moja ya maua mengi makubwa katika bustani iliyopo nyuma ya hili gorofa, nikabakiwa na bastola yangu pamoja na magazine za kutosha. Nikaanza kupanda kwa umakini kwa kutumia bomba la maji machafu lililo tengenezwa kwa chuma kizito. Nikafanikiwa kufika juu, taratibu nikasogeza dirisha hili la kioo, nikasikia miguno ya mapenzi ikitokea ndani ya hichi chumba. Nikachungulia vizuri nikamuona baba Hawa na Yudia wakila oroda huku mzee wa watu akijitahidi kuzungusha kiuno chake kwa utamu wa kum** anao pewa na Yudia. Nilipo muona mzee anazidi kuzungusha kiuno nikajua huu ndio wakati wa yeye kuweza kufunga goli hata la mkono. Nikaingia kupitia hapa dirishani ambapo ni dirisha la kioo na halina nando hata moja. Hadi ninasimama mbele ya kitanda chao ndio baba Hawa anamaliza kushangilia goli lake.
“Dany”
Yudia akawa mtu wa kwanza kukurupuka kitandani baada ya kuniona, baba Hawa akajaribu kuiwahi bunduki yake iliyopo pembeni ya kitanda chake, nikampiga risasi ya baga na kumfanya aanguke chini.Yudia akatulia kimya huku mwili mzima ukimtetemeka.
“Musiye mpenda amefika, muna la kuzungumza?”
Niliwauliza kwa ukali huku baba Hawa, akijitahidi kunyanyuka chini alipo angukia.
“Dany nakuomba unisamehe, haikuwa dhamira yangu ku…..kuu”
Yudia alizungumza kwa woga sana kwani uwepo wangu ndani ya chumba chao hawakuutegemea kabisa.
“Dany tunawahitaji wazima wote wawili”
Niliisikia sauti ya muheshimiwa raisi akizungumza kwa upole, hapakuwa na mtu yoyote aliye weza kuisikia ndani ya hichi chumba zaidi yangu peke yangu.
“Yupo wapi Hawa?”
“Umempa nini mwanangu mshenzi wewe”
Nikampiga risasi ya mguu baba Hawa na kumfanya agugumie kwa maumivu makali sana.
“Nimewauliza Hawa yupo wapi?”
“Ha…aha…awa. Nimemfu…ngia kwenye chumba chake”
“Muheshimiwa raisi, ninawaomba waingia, ila wahakikishe kwamba Hawa mtoto wa huyu firauni hapa wanamuoko”
“Nimekupata Dany, timu itaingia ndani ya dakika moja”
“Mshenzi unashirikiaana na wamarekani, wanakupa nini?”
Baba Hawa aliendelea kuzungumza huku akiwa ameyakaza meno yake kwa maumivu makali. Ndani ya dakika moja nikaanza kusikia milipuko huko nje pamoja na milio ya risasi ikirindima. Baba Hawa na Yudia wakazidi kuchanganyikiwa kwani kitu kinacho tokea hapa kinakwenda kuwashusha chini kwenye maisha yao yote.
Sikujaribu hata kukwepesha mboni ya macho yangu katika kuwaangalia baba Hawa na Yudia, ambao wote kwa pamoja wapo uchi kama walivyuo zaliwa. Galfa mlango ukafunguliwa kwa nguvu wakaingia wanajeshi wawili wa Al-Shabab, naamini wamekuja kwa ajili ya kumuokoa mkuu wao. Kwa haraka nikalala chini na kuwapiga risasi wakiwa katika harakati za kuingia ndani humu. Yudia akanirukia kutoka kitandani akiwa na kishu mkononi mwake. Kwa haraka kawahi kuishika mikono yake yote ili siku chake kisitue shingoni mwangu alipo kielekezea.
“Toka humu ndani mpenzi”
Yudia alizungumza huku akimuomba baba Hawa atoke ndani humu, ambaye taratibu akajitahidi kunyanyuka kutoka chini alipo kaa. Kusema kweli Yudia ana nguvu za mikono ambazo si rahisi kwa wanawake wengine kuwa nazo. Yudia akazidi kutumia nguvu katika kukishusha kisu chake, ila taratibu nikaanza kupata mafanikio ya kuigeuza mikono yake taratibu huku akinibana mbavu zake kwa miguu yake japo yupo uchi kabisa ila hakuna anaye jali utupu wake.
Nikamuona baba Hawa akitika katika chumba hichi huku akitembea kwa kwa kuchechemea, nikabana pumzi, nikaanza kunyanyuka chini nilipo lala chali huku Yudia akiwa amenikalia kiunoni mwangu. Nikafanikiwa kusimama nikatazama katika hichi chumba nikaona meza moja ya kiooa, nikatembea kwa mwendo wa taratibu huku nikiendelea kusikilizia maumivu ya mbaviu zangu zinavyo banwa na miguu ya Yudia aliyo izungusha kiunoni mwangu, huku mikono yangu ikiwa na kazi ya kukizuia kisu anacho hitaji kunichoma shingoni mwangu. Kwa Nguvu nikamshusha kwenye meza hii hadi ikavunjiaka na sote tukajikuta tukiwa tumeangukia kwenye hii meza ial Yudia ndio aliye tangulia chini kwa kuutanguliza mgongo wake. Yudia akapote nguvu ya kuhimili kukikamata kisu chake, ikawa ni rahisi kwa mimi kuweza kukishika kishu chake kwa mkono wangu wa kulia huku mkono wake wa kushoto ukiwa umeibana shingo yake kwa nguvu zangu zote.
“Imeisha sasa Yudia tutaonana ahera”
Kwa nguvu zangu zote nikakishusha kisu nilicho kishika kwenye sehemu zake za siri na chote kikazama ndani na kumfanya Yudia kutoa macho kwa maumivu makubwa. Sikutaka kuishia hapo nikachomoa kisu hicho kilicho jaa damu, nikakiandamiza kifuani mwake kwa nguvu, nikarudia kukishusha kwa mara nyinine ya pili. Mauaji ya familia yangu ya kikatili yakaanza kujirudia kichwani mwake.
“Ahahahahahahahahaaaaaghaaa”
Nilijikuta nikipiga kelele kwa nguvu na uchungu mkubwa huku nikikata kichwa cha Yudia pasipo huruma ya namna yoyote, damu nyingi zikanimwagikia kuanzia usoni mwangu ila sikulijali hilo hadi nilipo hakikisha kwamba nimekitenganisha kichwa na mwili.
“Dany Dany Dany”
Niliisikia sauti ya muheshimiwa raisi akiniita, sikumjibu kitu chochote zaidi ya mwili wangu kunitetemeka sana baada ya kuona nimekitengenisha kichwa cha Yudia na kiwiliwili cha mwili.
“Dany unatakiwa kutulia tafadhali, tulia Dany upo kwenye oparesheni unatakiwa kuiendelea, tafahdali tulia Dany”
Kumbukumbu ya Yudia jinsi nilivyo mkuta akicheza sebleni siku nilipo toka kulala hoteli ya mtendelea ikaanza kunijia kichwani mwake, uzuri alio barikiwa na mwenyezi Mungu ambao kusema kweli ulinipagawisha leo hii ndio umefikia mwisho tena kwenye mikono yangu. Nikajikuta nikizidi kutetemeka mwili wangu kwa woga sana, ni kazi rahisi kumuua mtu ambaye hujawahi kuwa naye kwenye mahusiano hata ya urafiki, ila ni ngumu sana kumua mtu ambaye ulisha wahi kuwa na mahusiano naye hata ya urafiki.
“Dany hadi sasa hivi tatufahamu ni wapi alipo mkuu wa Al-Shabab, tunakuomba uweze kurudi kwenye hali yako ya kawaida utusaidie kumpata huyu mzee”
“Muheshimiwa raisi”
Niliita taratibu huku machozi yakinimwagika usoni mwangu.
“Ndio Dany”
“Siwezi kuendelea na hii kazi”
“Hapana Dany, kumbuka kwamba hawa watu ndio walio kuulia wazazi wako, hawa ndio walimchinja dada yako Diana, hawa ndio walimchinja malaika wako mwanao Diana ambaye hakuwa na hatia yoyote, hawa ndio walio mchinja Mama yako na hawa ndio walio mteketeza mama wa mwanao, ni wakati wako sasa kuhakikisha kwamba wanalipa kwa damu za watu walio kufa pasipo makosa ya aina yoyote. Nyanyuka pambana, kumbuka uliniahidi kwamba uliniahidi kwamba utapambana hadi dakika ya mwisho na wala huto niangusha katika hili. Dany wewe ndio tegemezi langu kwa sasa, nimeiweka nchi yangu kwenye rahani ipo mikononi mwako. Akoa mamilio ya Wamarekani, okoa mabilioni ya Waafrika amba kila siku wanakufa kwa kunyanyaswa na majeshi wa kundi hili, watoto, wanamama wanakuwa wakimbizi kwenye nchi zao kwa ajilili ya hawa watu. Tafadhali Dany pambana”
Nilimsikia raisi anavyo zungumza kwa uchungu, huku sauti yake dhairi ikionyesha kwamba anamwagikwa na machozi. Nikaitazama bastola yangu iliyo anguka pembeni taratibu nikaichukua bastola yangu huku nikinyanyuka, nikazitazama damu zilizo mwagika chini za baba Hawa. Kwa haraka nikaanza kuzifwata sehemu zinapo elekea kwa kuzitazama kwa umakini. Damu hizi zikazidi kuniongoza, nikaanza kushuka chini kweneye ngazi za hili gorofa. Damu hizi zimeingia kwenye chumba kimoja, kwa haraka nikaupiga tege mlango wa chumba hichi na ukafunguka. Katika chumba hichi kuna ngazi zinazo elekea chini na kuna mwanga wa taa ndani ya chumba kilichopo chini ya ardhi. Kwa haraka nikaanza kushuka huku nikiwa bastola yangu.
Nikaona kordo ndefu iliyopo chini ya hii ardhi, michuruziko ya damu inaelekea mbele, nikaanza kukimbia huku nikiifwata kwa umakini sana.
Nikazidi kuongeza kasi kukimbiza kuelekea mbele kuhakiksiha kwamba ninampata baba Hawa, na kichwani mwangu sifikirii tena kumpa nafasi ya yeye kuweza kuishi na nikimpata nitahakikisha kwamba ninamuua kama nilivyo fanya kwa Yudia. Nikajibanza kwenye moja ya kona huku nikisikilizia miguu ya watu wanao kimbia kusonga mbele, nikachungulia taratibu, nikamuona Stive, Hawa, baba Hawa pamoja na wanajeshi wengine wanne wa Al-Shabab wakisonga mbele. Huku wanajeshi hao mara kwa mara wakiwa wanatazama nyuma kuimarisha ulinzi, kwa haraka nikapiga ishara ya msalaba huku nikishusha oumzi nyingi. Nikajitokeza na kuanza kuwafyatulia walinzi wa baba Hawa risasi ambao kusema kweli hapakuwa na hata mmoja aliye weza kujificha kwa maana sehemu waliyo kuwepo kwenye hii kordo hakuna sehemu yenye kona inayoweza kuwafanya wajifiche na mtu ambaye ninaweza kujificha ni mimi kutokana nipo kwenye kona inayo niwezesha kujibanza.
Nikazidi kuwaangusha walinzi wa baba Hawa ambao hawakuna na namna yoyote zaidi ya wao kuwa kizuizi cha risasi ambazo ninazipiga kwa baba Hawa, kitu nilicho weza kukigundua ni kwamba Hawa katika zoezi hili hakuweza kushiriki kabisa na anavyo onekena ameshikiliwa mateka. Stive akajiweka mbele ya baba Hawa huku bunduki yaki ikiwa imemuishia risasi baba Hawa hana bunduki yoyote, taratibu nikaanza kuwasogelea huku nikiwa nimeshika bastola yangu. Sikumuonea huruma Stive zaidi ya kumpiga risasi ya kichwa, akaanguka chini na kufa. Baba hawa kwa haraka amashika Hawa huku akiwa amempiga kabali, kadri nilivyo zidi kuwasogelea ndivyo nilizo zidi kuweza kuiona sura ya Hawa akiwa katika masikitoko makubwa sana huku machozi yakimwagika usoni mwake. Taratibu Hawa akaanza kutingisha kichwa chake akioniomba nisiwasogelee, nikayashusha macho yangu hadi kwenye mkono wake wa kushoto sikuamini macho yangu kuona alivyo shika bumo la mkono ambalo akifyatua kipini chake basi yeye na baba yake wanakwenda kulipuka na kuchanguka vipande vipande na huo ndio utakuwa ni mwisho wa maisha yao.
AISIIIII……….U KILL ME 129
“Dany nakuomba usije karibu”
Hawa alizungumza huku akiendelea kumwagikwa na machozi mengi sana usoni mwake.
“Hawa, tambua kwamba huna makosa yoyote, baba yako ndio ninaye muhitaji hapa. Tafadhali mke wangu, ninakuomba usifanya hicho unacho hitaji kukifanya kwa sasa”
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika usoni mwangu, sikutaka kusimama kama Hawa alivyo hitaji, nikazidi kutembea na kumsogelea ila bunduki yangu nikiwa nimeishika mkononi mwangu.
“Hawa nahitaji uishi karibu nami, nahitaji uwe mama wa watoto wangu, nahitaji tujenge familia, kumbuka fika mimi ndio mwanaume wako wa kwanza kuweza kuona mauongo yako ya ndani, ninafanya kila kitu kuhakisha kwamba ninakutunza, nina linda penzi lako, sina haja ya kuwa na mwanamke mwengine kama unanipenda ninakuomba usifanye chochote kibaya cha kukudhuru wewe”
“Hawa usimsikilize huyu ni muongo, lipua mwanangu bomu tufe”
Baba Hawa alizizungumza huku akiendelea kumkaba kabali Hawa, huku akiwa amejificha nyuma yake na ni ngumu sana kwa mimi kuweza kumpiga risasi baba Hawa kwani Hawa ndio kizuizi chake.
“Hawa kumbuka ni mangapi tuliyapanga, kwa nini unahitaji yaishe kwa namna hii, kwa nini unahitaji maisha yaende namna hii, tafadhali Hawa ninakuomba sana mke wangu”
“Mwanangu huwezi kufa mikononi mwa Wamarekani, anakudanganya huyo ni mjinga mshenzi, kumbuka mama yako hata huko mbinguni anasubiri kuwa pamoja nasi, lipua bomu”
Baba Hawa alizidi kuzungumza kwa msisitizo na kuzidi kumfanya Hawa amwagikwe na machozi mfululizo. Hawa akanitazama kwa macho yaliyo jaa huruma sana, kwa nguvu akamgeukia baba yake na kumkumbatia, mkono ulio shika bomu nikaona akiuingiza kwenye koti hili alilo vaa baba yake. Hawa akamsukumia baba yake pambeni na yeye akakimbilia upande wangu na sote tulalala chini huku nikiwa juu yake nikimfunika. Mlipuko mkubwa ukatokea huku vipande vya nyama nyama pamoja na damu vikiniangukia mgongoni mwangu.
Taratibu nikageuka na kutazama eneo alilo simama baba Hawa, nilicho kiona kimesalia ni kobazi alizo kuwa amezivaa tu, tena nazo zimekatika katika. Hawa akaka kitako huku akilia kwa uchungu sana, kwa nguvu nikamkumbatia huku nami machozi yakinimwagika.
“Yameisha mke wangu”
Nilizungumza huku nikimkumbatia kwa nguvu Hawa.
“Dany nimemuua baba”
“Hapana baby ilibidi iwe hivyo tu”
Nilizungumza huku nikiendelea kumkumbatia Hawa kifuani mwake.
“Dany kazi nzuri”
Niliisikia sauti ya muheshimiwa raisi akizingumza nami. Taratibu nikasimama, nikamsaidia Hawa kusimama, kwa mikono yangu miwili nikambeba Hawa na kuanza kutembea naye kuelekea nje. Tukakutana na baadhi ya wanajeshi wa Kimarekani ambao tayari wamesha weza kuiweka ngome chini ya ulinzi mkali, huku wanajeshi wengi wa baba Hawa wakiwa wameuwawa. Mwanajeshi mmoja akanisaidia kumbeba Hawa na kumuwahisha katika gari la jeshi linalo shuhulikia wagonjwa.
“Muheshimiwa raisi unanisikia?”
“Ndio Dany ninakusikia”
“Ninakuomba mke wangu Hawa umlinde kwa kila jinsi yeye ndio furaha yangu na wala siweza kuwa na furaha nyingine zaidi yake yeye”
“Nakuahidi Dany, nitahakikisha kwamba ninamlinda mpenzi wako, na hakuna jambo lolote litakalo mfika”
“Nashukuru muheshimiwa raisi, ninakuambini katika hilo”
Nikamtazama Hawa aliye lazwa kwenye kitanda cha wagonjwa, huku madaktari hawa wa jeshi wakiendelea kumpa huduma ya kwanza.
“Dany”
Hawa aliniita kwa sauti ya upole sana huku akinitazama usoni mwangu.
“Ndio mke wangu”
Nilizungumza huku nikiinama taratibu huku nikimtazama Hawa usoni mwake.
“Umefanya kazi kubwa sana”
“Bila ya wewe kuwa moyoni mwangu wala nisinge weza kuifanya hii kazi peke yangu, nimefanya haya yote kwa ajili yako mke wangu”
“Natambua hilo Dany, ninakupenda sana”
“Ninakupenda pia mke wangu”
“Dany, tunatakiwa kumpeleka mke wako hospitali kwa matibabu zaidi”
Mwanajeshi mmoja alizungumza huku akiwa amesimama mbele yangu, taratibu nikauchanisha mdomo wangu na mdomo wa Hawa.
“Munampeleka hospitali gani?”
“Katika kambi yetu ya Jeshi hapa Somali”
“Sawa”
Wanajeshi hawa wakambeba Hawa katika kitanda hichi cha wagojwa, wakamuingiza katika helicopter moja kati ya Helicopter nne za jeshi zilizopo katika hili eneo na taratibu ikaacha ardhi na kuondoka.
“Muheshimiwa raisi, oparesheni ya kufuta jeshi la Al-Shabab, imekwisha”
“Nashukuru Mungu. Dany sasa unaweza unaweza kwenda kwenye kambi ya jeshi la Marekani hapo Somalia”
“Sawa muheshimiwa raisi, ila inabidi kuendelea na opareshni ya kuwasaka Boko Haramu”
“Ni kweli ila unabidi upumzike kidogo”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Nikaingia kwenye moja ya helicopter safari ya kuelekea katia kambi ya jeshi la Marekani hapa Somalia ikaanza. Sikuamini kwamba nimeweza kulipiza kiasi changu kwa asilimia ishirini na tano na hadi sasa hivi nimebakisha alisiliami sabini na tano ambazo bado sijafahamu kwamba ninazimaliza vipi. Hatukuchukua muda mwingi sana tukafanikiwa kufika katika kambi ya jeshi la Marekani hapa Somali.
“Ninahitaji kumuona mke wangu”
Nilimuambia mkuu wa hii kambi aliyo kuja kunipokea hapa.
“Sawa twende huku”
Tukapanda katika gari ndogo ya jeshi ambayo haijafunikwa kwa juu. Tukaondoka katika eneo hili la uwanja wa ndege za kijeshi. Kambi hii ina majengo mengi sana na ulinzi wake ni mkali sana.
“Umefanya kazi nzuri Dany”
“Nashukuru”
“Wewe utaifa wako ni Tannia?”
“Ndio”
“Kwa nini usichukue uraia wa Marekani, na ukafanya kazi chini ya Marekani?”
“Hahaaa, mimi ni muafrika na ni Mnzania halisi, kwa hiyo siwezi kubadilisha utaifa wangu”
“Sawa ni ombi tu niliko kuwa nina kuomba”
“Nimekuelewa meja”
Tukafika kwenye moja ya jengo, tukashuka kwenye gari hii, Tukaongozana hadi kwenye moja ya chumba. Meja akanifungulia mlango na nikaingia ndani kisha yeye akabaki nje, nikamkuta Hawa akiwa amelala kitandani huku ametundikiwa dripu la maji. Taratibu nikavuta kiti kilichopo karibu na kukaa karibu yake huku nikimtazama osoni mwake.
“Unaendeleaje mke wangu?”
“Safi tu”
Nikavua kinasa sauti sikioni mwangu na kukiweka mfukoni mwangu, nikavua pia kofia yangu na kuiweka pembeni.
“Pole honey”
“Asante mke wangu, vipi wamekuambia una tatizo gani?”
“Ni maji tu yamepungua mwilini mwangu, ila kila kitu kipo vizuri”
“Nafurahia kusikia hivyo”
“Vipi uliweza kumdhibiti Yudia?”
“Ndio, niliweza kumdhibiti, na kwa sasa amekufa”
Taratibu Hawa akashusha pumzi yake, akanishika mkono wangu wa kulia na kuuweka kifuani mwake.
“Moyo wangu kwa sasa una amani sana kwa sasa, umenifanya maisha yangu kubadilika. Kwa sasa Dany ninacho kifikiria ni kuwa mama, na mimi nina hitaji kuwa mwanamke mwenye familia yangu, watoto wangu”
Hawa alizungumza kwa hisia kali sana huku akiwa amejawa na tabasamu zuri usoni mwake, lililo nifanya na mimi kujihisi furaha kubwa.
“Nashukuru kwa kulifahamu hilo mke wangu, nitahakikisha ninakulinda wewe hadi mwisho wa maisha yangu”
“Asante baby”
Nikambusu Hawa kwenye paji la uso wake na furaha kubwa ikazidi kutawala katika mioyo yetu na ninaamini kwamba ukurasa mpya wa maisha umefunguliwa katika maisha yetu. Hawa akaniomba nikilaze kifua changu kifuni mwake, nikafanya hivyo, usingizi kwa mbali ukaanza kunipitia na kujikuta nikilala fofofo.
“Dany, Dany”
“Mmmm”
“Kumekucha mume wangu”
Hawa alizungumza na kunifanya ninyanyue kichwa changu. Nikamkuta nesi akiwa amesimama pembeni yetu
“Umeamkaje mke wangu”
“Nipo poa, nesi anahitaji kunihudumia”
“Ahaa”
Nilizungumza huku nikinyanyuka, nikaanza kujinyoosha viungo vyangu kwa maana nimechoka sana kwa kazi ngumu niliyo ifanya kwa siku hizi nne.
“Nesi mke wangu hali yake vipi?”
“Yupo vizuri, ila maji tu ndio yalimpungua mwilini mwake”
“Sawa”
“Ila dripu hili ninalo muwekea ndio la mwisho baada ya hapa atakuwa salama”
“Sawa”
Nikasimama dirishani na kutazama nje, nikaona wanajeshi wakiwa katika mazoezi huku wengine wakikimbia mchaka mchaka katika mistari iliyo nyooka. Mlango ukafunguliwa akaingia meja wa jeshi aliye nipokea jana.
“Habari za asubuhi Dany”
“Salama”
“Kuna simu yako kutoka kwa muheshimiwa raisi”
“Naiomba”
Nikaichukua simu ya mkononi aliyo kuja nayo huyu meja, niakiweka sikioni mwangu huku nikimtazama Hawa usoni mwake.
“Muheshimiwa raisi”
“Habari za asubuhi kwa uko Somalia?”
“Salama muheshimiwa raisi”
“Sasa kazi ya kwenda nchini Nigeria imeanza ila nitahitaji uwende kama mpelelezi, na kazi ya kuhakikisha kwamba unagundua ni wapi makao makuu ya Boko haramu itakuwa mikononi mwako”
Taratibu nikashusha pumzi huku nikimtazama Hawa usoni mwake.
“Sawa muheshimiwa raisi”
“Ila Dany nina ombi moja?”
“Ombi gani?”
“Katika hii oparesheni, mke wako Hawa aweze kuhusika nina imani atakuwa anafahamiana hata na baadhi ya viongozi wa kundi hilo na itakuwa ni rahisi sana kwenu katika hii kazi”
“Ila muheshimiwa raisi, mke wangu kwa sasa hali yake sio nzuri sana ya kuweza kumfanya aifanye hii kazi”
“Dany”
Hawa aliniita huku akinitazama usoni mwake.
“Naomba nizungumze na muheshimiwa raisi”
“Sasa hivi?”
“Ndio”
Nikamtazama meja pamoja na huyu nesi, nikamsogela Hawa.
“Muheshimiwa raisi mke wangu anahitaji kuzungumza na wewe”
“Mpe simu”
Taratibu nikampa simu Hawa, akaweka loudspeaker na kutufanya sote tusikie mazungumzo yake na raisi.
“Muheshimiwa raisi sasa unazungumza na mrs Dany”
“Ndio Mrs Dany, nimemuomba mume wako muweze kuungana naye katika oparesheni ya kwenda nchini Nigeria, huko mutakuwa katika uchunguzi wa kufwatilia kundi zima la Boko Haramu, nina imani kwamba unaweza kufahamu baadhi ya viongozi ambao wanamiliko kundi hilo”
Nesi akatoka ndani ya chumba hichi na kutuacha sisi watatu.
“Nimekuelewa muheshimiwa raisi, ninamfahamu mtoto wa kiongozi mkuu wa hilo kundi, naamini kupitia yeye kazi inaweza kukamilika kwa kiasi fulani”
“Nashukuru kusikia hivyo mrs Dany”
“Ila mimi sinto kwenda, nitatoa maelekezo ambayo nina imani kwamba mume wangu anaweza kuifanya hii kazi pake yake”
Kidogo nikajikuta nikishusha pumzi nikimshukuru Mungu kusikia kwamba Hawa hato jihusisha kabisa na oparesheni hii.
“Sawa mrs Dany ni maelekezo yapi hayo?”
“Kwa sasa siwezi kuyatoa, hadi niweze kuwa katika sehemu salama na ya kuaminika”
“Sehemu gani unahitaji kuwa Mrs Dany?”
“Ninahitaji kuishi kwa kipindi chote cha hii oparesheni ya mume wangu hapo ndani ya ikulu yako, naamini Dany atakuja kunichukulia hapo akimaliza kazi yake.”
Maeno ya Hawa yakatufanya mimi na meja kutazamana kwani sikutegemea kama Hawa anaweza kuomba kuishi katika ikuli ya raisi wa Marekani, ambayo inasifika sana kwa kuwea kulindwa kuliko ikulu yoyote Duniani.
==>>ITAENDELEA KESHO
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment