Septemba 28 ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa msanii Wema Sepetu ambapo Leo ameandaa tukio maalum kwaajili yake litakalofanyika pale Mlimani City.
Tukio hilo litaambatana na uzinduzi wa filamu yake aliyofanya na Van Vicker kutoka Ghana ambaye yupo tayari nchini Tanzania.
Katika kuifanya siku hiyo kuwa nzuri, Wema amefanya interview na vituo mbalimbali vya habari ambapo siku ya jana kupitia ThePlaylist ya Times FM alifunguka kuzungumzia kama aliwahi kwenda kwa mganga katika maisha yake.
“Hapana sijawai kwenda lakini nimekuwa nikinywa sana mitishamba kwaajili ya tatizo langu la kukosa mtoto, nimekunywa sana mpaka wanahisi zimeniongezea tatizo,” alisema Wema Sepetu.
Mrembo huyo amedai tataizo la kutopata mtoto ndio kitu ambacho kimekuwa kikimsumbua kwa muda mrefu huku akidai baadhi ya wabaya wake wamekuwa wakitumia hiyo kama njia ya kumuumiza.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment