Uzinduz FlyOver: Rais Magufuli Ammwagia Sifa Mfugale

Rais John Magufuli, amewataka wataalamu nchini kuiga uchapakazi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) Patrick Mfugale, kwa kuwa waaminifu na kutanguliza Utanzania kwanza.

Ameyasema hayo leo Septemba 27 katika sherehe ya uzinduzi wa daraja la juu la Mfugale lililopo katika makutano ya Barabara ya Mandela na Nyerere eneo la Tazara jijini Dar es salaam ambapo amesema kwa uaminifu wa Mfugale hauwezi ukasahaulika kamwe.

“Wataalamu wa Tanzania wasiwe chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu kwani badala yake waige uchapakazi wa Mfugale yeye hakupendelewa bali alitanguliza Utanzania mbele badala ya ubinafsi,” amesema.

Amesema kutokana na changamoto na hatua mbambalimbali alizozifanya Mfugale tangu mwaka 1977 akiwa mhandisi Wizara ya Ujenzi, ana imani Watanzania watakubaliana naye kuwa daraja hilo lilistahili kupewa jina lake.

“Ninampongeza Waitara (Mbunge mteule Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara) kwa kurudi kwani maendeleo hayana chama sijasema wote waje siwahitaji ila wale ambao wanaosumbuka na mizigo waje tutawakaribisha kwa mikono miwili tujenge maendeleo ya nchi yetu.

Daraja hilo lililopewa jina la ‘Mfugale Flyover’ limegharimu Sh bilioni sita iliyohusisha usimamizi wa ujenzi wenyewe, limejengwa kwa nguzo kubwa 26 na uwezo wa kubeba tani 180 kwa wakati mmoja pia lnatarajiwa kudumu zaidi ya miaka 100.


from MPEKUZI

Comments