Mashabiki wamekuwa na maswali mengi ni kitu gani anapitia Lady Jaydee kwa sasa kwenye maisha yake.
Hii ni kutokana na kuandika ujumbe akieleza jinsi alivyotaka kukatisha uhai wake ghafla. Kupitia mtandao wa twitter ameandika;'
"Jana nilihisi kunywa sumu ila kabla sijafanya nikajisuta na kujikumbusha nilipotoka na kujiuliza nitakuwa mjinga kiasi gani 😔😔 Nikajisikitikia tu kisha nikaacha. Na leo bado nipo kigumu gumu ila bado nipo"
Muimbaji huyo kwa sasa yupo kwenye maandalizi ya show yake inayokwenda kwa jina la Vocals Night ambayo itafanyika August 26, 2018 Milimani City, Dar es Salaam.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment