Chadema kumshtaki Waitara Kamati ya Maadili

Chama cha Demokrasia Maendeleo (Chadema) kimempeleka kwenye kamati ya maadili mgombea ubunge wa jimbo la Ukonga kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara kwa kile walichodai kufanya uchochezi.

Akizungumza leo Agosti 29, mkurugenzi wa oparesheni na mafunzo wa Chadema, Dingo Kigaila kuwa amesema sababu ya kumpeleka kwenye kamati hiyo ni kutokana na madai ya kuhamasisha vurugu kwa kupitia mtandao wa kijamii.

Amesema kwa kutumia simu yake ya kiganjani Agosti 26 mwaka huu aliandika kwamba watu wa kabila lake yaani Wakurya hususani ukoo wa Wairegi wanoe mapanga yao na kumwaga damu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi jimbo la Ukonga.

Amesema Waitara alitumia lugha ya Kiswahili na Kikurya kuandika ujumbe huo, hivyo wameitaka kamati ya maadili, kumuita na kumuhoji mgombea huyo.

Julai 28, 2018 Mwita Mwikwabe Waitara, alitangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na kujivua nyadhifa zake zote ndani ya CHADEMA na kuhamia CCM.


from MPEKUZI

Comments