Mfanyabiashara Said Lugumi na mmiliki wa Kampuni ya Lugumi Enterpreises Limited, amejisalimisha polisi kuitikia wito wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola aliyemtaka kujisalimisha kwake ndani ya siku 10.
Lugumi aliwasili katika Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi leo asubuhi Julai 31, ikiwa ni siku 10 tangu Waziri Lugola atoe agizo hilo Julai 21, mwaka huu.
Mfanyabiashara huyo aliongozwa na Ofisa wa Polisi kuelekea ofisini kwa Waziri Lugola baada ya kutoka Makao Makao Makuu ya Polisi Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai.
Julai 21, mwaka huu Lugola alitoa agizo akimtaka mfanyabiashara huyo kujisalimisha ili azungumze naye kuhusu kazi aliyopewa lakini hata hivyo hakuimaliza.
Kampuni ya Lugumi ilitekeleza mradi wa kufunga mfumo wa utambuzi wa alama za vidole katika vituo vya polisi uliogharimu Sh bilioni 37.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment