Kauli ya Lowassa Baada ya Mbunge wa CHADEMA Jimboni Kwake Kujiuzulu na Kuhamia CCM

Muda mchache baada ya Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga (Chadema), kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amewataka wananchi jimboni humo wasife moyo na kuwa na utulivu.

Lowassa ambaye pia amewahi kuwa Mbunge wa Monduli kabla ya Kalanga, amesema amesikia taarifa za kujiuzulu kwa mbunge huyo na kwamba kwa sababu zozote ambazo amezitoa ni haki yake kikatiba.

“Najua Wana-Monduli wote nikiwamo mimi uamuzi huo umetuhuzunisha na kutuumiza, lakini nawaomba msife moyo hata dakika moja zaidi kitendo hicho kizidi kutupa nguvu, ari, hamasa na mori zaidi ya kuendeleza mapambano ya kuitafuta demokrasia na mabadiliko ya kweli.

“Hakuna jipya katika hili, ni kawaida kwa wanasiasa duniani kuhama vyama vyao na kubadilishana vijiti. Monduli imetupa heshima kwenye harakati za mabadiliko, naomba msife moyo,” amenukuliwa Lowassa ambaye pia ni Mjumbe Kamati Kuu ya Chadema.


from MPEKUZI

Comments