Ofisa Utumishi Mkuu Wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Atoa Ushahidi Mahakamani Dhidi ya Mtumishi Wao Anayedaiwa Kumiliki Mali Nyingi
Ofisa Utumishi Mkuu Wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Evans Emil ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Ofisa Msaidizi wa Forodha wa TRA Jennifer Mushi anayedaiwa kumiliki magari 19 yasiyolingana na kipato chake anamiliki baadhi ya mali asilimia 50 kwa 50 na familia yake.
Emil ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ameyaeleza hayo wakati akijibu maswali ya wakili wa serikali Pius Hilla mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.
Katika ushahidi huo Emil amedai kuwa July Mosi, 2011 Jennifer alipewa ajira na kupatiwa fomu mbalimbali ajaze ikiwamo fomu ya Tamko ya Rasilimali na madeni. Katika fomu hiyo ya rasilimali March 30,2012 imeonyesha Jennifer anamiliki fedha taslimu Sh.Laki 6 zilizopo katika benki na taasisi za fedha Sh 800,000.
Pia alikuwa na Hisa na gawio la thamani ya Sh.Laki 6, anamiliki nyumba Kinyerezi Kichangani ya Sh.Mil 30 ambapo anamiliki asilimia 50 kwa 50 baina yake na mumewe, vilevile anamiliki shamba la Heka 1 Mabwepande lenye thamani ya Sh.Laki 7, ambapo anamiliki asilimia 50 kwa 50 baina yake na mumewe.
Pia anamiliki Kiwanja Heka 1 Kigamboni thamani yake ni Sh.Mil 9 ambapo umiliki wake wake asilimia 50 kwa 50 na mumewe Pia anamiliki gari aina ya Van T 884 BNU thamani Sh.Mil 8 umiliki wake asilimia 50 na mume asilimia 50.
Katika fomu ya tamko ya rasilimali na madeni ya February 20, 2013 alikuwa na fedha taslimu Sh. Laki 8 pamoja fedha zilizopo taasisi za fedha ni Sh.Mil 1, nyumba Kinyerezi thamani ya Sh.Mil 35 ambapo umiliki wake ni asilimia 50 kwa 50 na mumewe.
Pia anamiliki Kiwanja eneo la Bunju thamani ya Sh.Mil 1.7, pia kiwanja kilichopo Kigamboni thamani ya Sh.Mil 9 ambacho wanamiliki ni watoto wake.
Pia ana magari mawili aina ya RV4 moja ikiwa na thamani ya Sh.mil 8 na jingine Sh.Mil 13 ambapo umiliki wake asilimia 50 kwa 50 na mumewe.
Katika fomu ya tamko ya rasilimari na madeni ya December 11,2015 inaonyesha ana fedha taslimu benki Sh. Laki 5 na katika taasisi za fedha Sh.Mil 2.7, Pia ana kiwanja Kigamboni cha Sh.Mil 9 ambapo umiliki wake wake ni asilimia 50 kwa 50 na mumewe.
Pia ana magari mawili aina ya Toyota moja ni Sh.Mil 18 na jingine Sh.Mil 14.Pia ana Deni la saccos ya TRA la Sh.Laki 6. Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi June 6,2018 ili kuendelea na shahidi wa pili.
Katika kesi hiyo mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa kati ya March 21,2016 na Juni 30,2016 jijini Dar es Salaam akiwa mwajiriwa wa TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akimili magari 19 yenye thamani ya Mil.197 kinyume na kipato chake halali. Pia amekutwa akiishi maisha ya kifahari yenye thamani ya Sh.Mil 333 fedha ambayo hailingani na Kipato chake halali.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment