Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira imesema changamoto iliyopo katika kupata taarifa sahihi za Wazanzibar wanaopata ajira katika Taasisi za Muungano anuani ya makazi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Kangi Lugola amesema hayo bungebi jijini Dodoma leo Mei 30, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Welezo, Saada Mkuya (CCM).
Katika swali lake, Mkuya huyo alitaka kujua katika mambo yaliyokubalika katika mkakati wa kutatua changamoto za Muungano.
“Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na kugawana ajira zilizopo katika Taasisi za Muungano kwa asilimia 21 Zanzibar na 79 kwa Tanzania Bara, je ni kwa kiasi gani mkakati huo umetekelezwa,” aliuliza Mkuya.
Akijibu swali hilo Lugola amesema: “Changamoto iliyopo katika kupata taarifa sahihi za Wazanzibar wanaopata ajira katika Taasisi za Muungano ni kutoandika anuani zao za Zanzibar badala yake wanatumia anuani za mikoa ya Tanzania Bara.”
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment