Kauli Ya Kitila Mkumbo Kuhusu Katibu Mpya wa CCM

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Bashiru Ally ni mtu sahihi kwa zama za sasa kuwa katibu mkuu wa chama hicho tawala.

Jana Halmashauri Kuu, ambayo ni chombo cha pili kwa ukubwa cha CCM ilikutana kwa siku mbili Ikulu jijini Dar es Salaam, na kumpitisha msomi huyo ambaye aliongoza kamati iliyohakiki mali za chama hicho kwa miezi mitano, kuwa katibu mkuu.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter Profesa Mkumbo amesema, “katika kipindi ambacho silaha ya siasa ni nguvu ya hoja, weledi, na uimara CCM imepata katibu mkuu sahihi kwa zama sahihi nakutakia mafanikio makubwa komredi Dk Bashiru Ally.”

Uteuzi huo umekuja baada ya aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana kuandika barua ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli.



from MPEKUZI

Comments