Na Mahmoud Ahmad Dodoma
Imeelezwa kuwa hapa nchini TANZANIA hutumia zaidi ya dola milioni 200 sawa na bilioni 400(Mutungi and Affognon 2013) kuangiza chakula kutoka nje ya nchi kila mwaka hali inayosabaisha wakulima wadogo wadogo kulazimika kuuza mazao yao kwa bei ya nchini.
Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Afisa habari wa wakulima wadogo Tanzania Flora Mlowezi wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya kilimo na kamati ya bunge kilimo, mifugo na maji uliofanyika bungeni jijini Dodoma.
Mlowezi alisema wakulima wanalazimika kuuza mazao kwa bei ya chini kwa sababu ya uwezo mdogo kwenye usimaminzi wa mazao baada ya mavuno.
Aliongeza kuwa katika Afrika Mashariki ni asilimia tano tu ambayo huwekezwa kwenye usimaminzi wa mazao baada ya mavuno na asilimia 95 hutumika katika uzalishaji.
‘’Thamani ya upotevu kwenye nafaka kwa mwaka ni zaidi ya dola milioni nne sawa na bilioni nane (Rockeffer foundation)’’alisema.
Alifafanua kuwa zaidi ya asilimia 70 ya wanawake wa Tanzania wanahusika katika uzalishaji wa mahitaji ya chakula pia sera ya Taifa ya kilimo ya mwaka 2013 imesema zaidi ya asilimia 90.4 ya wanawake wa Tanzania wanajihusisha na shughuli za kilimo na kutimiza lengo namba mbili la ajenda ya malenho endelevu (2030).
‘’Wengi wao ni wakulima wadogo ambao hawana uwezo wa kuendesha shughuli za kilimo kwa ufasaha kutokana na changamoto mbalimbali kama upatikanaji wa pembejeo kwa wakati na kwa bei nafuu, ukosefu wa taarifa, mitaji na kufikiwa na huduma za ugani pamoja na uhakika wa ardhi,’’alisema Mlowezi.
Naye msemaji wa shirika lisilo la kiserikali la Action Aid Joram Wimmo alisema katika bidhaa ya maziwa bado upo uwezekano wa kuzalisha zaidi kutokana na hivi sasa kuwa katika kiwango cha chini.
Alisema hivi sasa kuna viwanda 75 vya maziwa vyenye uwezo wa kusindika lita 672,000 kwa siku , uwezo wa sasa kwa siku ni lita 155,450 sawa na asilimia 23.3 kwa siku.
‘’Maziwa yanayozalishwa ni wastani wa lita bilioni 2.2 kwa mwaka, kati ya hayo ni asilimia 10 tu ndiyo yanayoingia katika mfumo rasmi wa soko kutokana na kiasi kidogo kinachosindikwa nchini bado tunatumia kiasi cha Sh. bilioni 23.6 kuagiza maziwa nje ya nchi kwa mwaka,’’ alisema Wimmo.
Wimmo aliiomba serikali kutenga fedha ya kutosha ili kuboresha huduma za ugani na pembejeo ,serikali kutekeleza miongozo kwa kuzingatia ikama ya kila kijiji kwa kila watu 600 awepo afisa ugani mmoja au zaidi.
Mara baada ya kupokea taarifa hiyo wabunge wa kamati ya kilimo, mifugo na maji akiwemo mwenyekiti wa kamati hiyo Christine Ishengoma alisema wameipokea taarifa hiyo na kuahidi kuifanyia kazi na kuishawishi serikali kuongeza bajeti ili kuweza kutatua changamoto hizo.
Lengo la mkutano huo ni kuwasilisha mapendekezo ya wakulima kwa kamati ya kilimo, mifugo na maji ili waishauri Serikali kutwenga bajeti yakutosha ili kuwepo na uboreshwaji wa miundombinu kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment