Serikali kupiga marufuku uagizwaji wa Mita za Luku kutoka nje ya nchi

 Waziri wa Nishati, Dr. Medard Kalemani amesema kuanzia July 1,2018 serikali itasitisha rasmi uagiziaji wa mita za Luku ya umeme kutoka nje ya nchi ili kutoa fursa kwa wawekezaji wa ndani.

Dr. Kalemani ameyasema hayo wakati akizindua kiwanda cha kutengenezea mashine za Luku maeneo ya Mbezi, ambapo amesema uwepo wa wawekezaji wa ndani utaokoa muda na kupunguza gharama hasa katika sekta hiyo ya nishati.

Amesema kuwa usitishwaji huo ulitanguliwa na ule wa awali ambapo walisitisha uingizaji wa nguzo za umeme kutoka Afrika Kusini na Transformer kutoka India.

Amesema kuwa kuna faida nyingi kwa Mita hizo kutengenezwa nchi ikiwemo kuokoa muda wa uagiziaji na kupunguza gharama.

“June 2017 tulisitisha rasmi uingizaji wa nguzo kutoka Afrika Kusini, ambapo nguzo moja tulikuwa tunanunua Laki 3 hadi Laki 4, wakati ukinunua nguzo za hapa ndani ni Laki 2” amesema Kalemani

” Shirika la Tanesco limekuwa na mizigo mikubwa kwa sababu ya gharama ya kuagizia vifaa kutoka nje ya nchi,”-Kalemani

Pia Dr. Kalemani amesema kuna tatizo la ubora, kwani kuna baadhi ya nchi zina majina makubwa lakini bidhaa zao feki, kwani mwaka jana ziliungua transformer 100 kutoka India kwa wakati mmoja.


from MPEKUZI

Comments