Rais John Magufuli amewataka wanakijiji cha Migori mkoani Iringa kutumia barabara ya lami ya Iringa-Dodoma kujitajirisha.
Akizungumza leo Jumapili Aprili 29, aliposimama kwa muda katika kijiji cha Migori wakati akielekea Iringa, Rais Magufuli amewataka wanakijiji hao kuchapa kazi.
“Barabara imekamilika mnaiona, itumieni ili mtajirike, limeni mazao kwa bidii na msafirishe kwenda sehemu mbalimbali za nchi,” amesema Rais Magufuli.
Aliwataka kutumia mvua zinazoendelea, kulima na kufuga ili waweze kunufaika.
Rais Magufuli atakuwa na ziara mkoani Iringa ambako Jumanne Mei mosi atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zitakazofanyika kitaifa mkoani Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amesema sherehe hizo zitahudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai, mawaziri na wabunge.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment