Mkuu wa Mkoa wa Dodoma abainisha ubadhirifu mradi wa maji

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amesema kuna ubadhirifu wa Sh1.5 bilioni kwenye mradi wa maji katika wilaya za Kondoa na Chemba ambao unasuasua.

Dk Mahenge amesema hayo leo Aprili 27 Kondoa, Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa barabara ya Kondoa – Babati yenye urefu wa kilomita 251 inayozinduliwa na Rais John Magufuli.

Mkuu huyo wa mkoa amesema mradi huo ulitengewa Sh2.8 bilioni kwa ajili ya wilaya hizo lakini kulitokea ubadhirifu wa Sh1.5 bilioni. Amebainisha kwamba vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi wa ubadhirifu huo.

“Tayari vyombo vya dola vinafanya uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha hizo. Dhamira ya Serikali iko pale pale kuhakikisha kwamba maji yanapatikana katika mkoa wa Dodoma,” amesema mkuu huyo wa mkoa.

Dk Mahenge amesema Serikali imetenga Sh70 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika mkoa huo. Amesema kwenye sekta ya maji, Serikali imeanza ujenzi wa visima vitano ambavyo vitasaidia kukidhi mahitaji ya maji katika mkoa huo.


from MPEKUZI

Comments