Mbunge Alalamika Kuminywa na Kiti Bungeni

Katika hatua isiyo ya kawaida leo Bungeni Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ametoa mwongozo akitaka viti vya bungeni kukarabatiwa kwa kuwa viti hivyo ni vibovu na vinawapa shida wabunge.

Salasini ameyasema hayo kwenye kipindi cha Maswali na majibu huku mwongozo wake ukiitaka serikali itoe majibu ni lini viti hivyo vitakarabatiwa ili kuwaondolea adha wabunge wakati wa vikao.

''Mh. Spika viti hivi tunavyokalia havipo kwenye hali nzuri kabisa, vimechakaa na havifanyiwi marekebisho na leo kiti changu kimenifinya makalio. Je ni lini vitafanyiwa ukarabati ?,'' amesema Selasini.

Baada ya kuomba muongozo huo Spika wa Bunge Mh. Job Ngudai amesema kuwa suala hilo limepokelewa na litatolewa ufafanuzi.


from MPEKUZI

Comments