Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe ameripoti Kituo Kikuu cha Polisi saa nane mchana na kuondoka saa 8.20 mchana.
Vingozi wengine walioripoti ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Bunda Ester Bulaya , mbunge wa Tarime, Ester Matiko na Naibu Katibu Bara, John Mnyika.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilitoa dhamana kwa viongozi hao Machi 27 na kuwapa sharti la kuripoti kituo kikuu kwenye ofisi ya RPC kila Ijumaa.
Viongozi ambao hawajafika mpaka sasa ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Mbunge wa Tarime, Vijijini, John Heche.
Viongozi hao kwa mara ya kwanza walipokea wito Februari 20, Jeshi la Polisi likiwataka kufika kituoni hapo baada ya maandamano ya Februari 16.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment