Mbunge wa Chalinze kupitia CCM, Mh. Ridhiwani Kikwete ameonesha kuridhishwa na kazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli hususani katika kuboresha miundombinu nchini.
Ridhiwani ameyasema hayo baada ya kujionea ub ora wa daraja la Kelema wilayani Chemba mkoani Dodoma, alipopita eneo hilo ikiwa ni sehemu ya safari yake kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya Muungano yaliyofanyika jijini humo.
Kupitia mtandao wa Twitter Mh. Ridhiwani ameandika, ''Nikiwa na mke wangu, kuangalia uzuri wa nchi yetu. Hakika ni nchi nzuri yenye kuvutia. Hongera sana Rais wangu @MagufuliJP kwa kusimamia Miundombinu, pia Asante @WorldBankAfrica kwa kusaidia maendeleo''.
Aidha katika ujumbe huo wa Ridhiwani pia ameishukuru Benki ya Dunia kwa misaada inayotoa hususani ujenzi wa barabara ambao ndio umekuwa kipaumbele chake katika nchi zinazoendelea ikizisaidia kwa mikopo ya masharti nafuu.
April 27 Rais Magufuli alizindua barabara ya Kondoa-Babati, yenye urefu wa Km 251. Katika uzinduzi huo aliwataka wananchi kutunza miundombinu hiyo, haswa alama za barabarani kwani hiyo ndio barabara kuu kwa upande wa Kaskazini.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment