CCM yakomba safu nzima ya uongozi Chadema

Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ediwn Sanda amesema kuwa safu ya uongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye jimbo hilo wamehamia CCM kutokana na kazi nzuri anazozifanya Rais Dkt. Magufuli

Ameyasema hayo leo April 27, 2018 alipopata nafasi ya kuwasalimu viongozi mbalimbali akiwemo Rais Dkt. Magufuli kwenye sherehe za ufunguzi wa barabara ya Kondoa, Babati yenye urefu wa kilomita 251

“Rais safu ya uongozi mzima ya CHADEMA imehamia CCM, Mwenyekiti wa Jimbo, Katibu wa Jimbo, na viongozi wengine kwa uchache wao, kwa kweli nashukuru sana ila tunakwenda kubomoa moja kwa moja dhana ya upinzani Kondoa kwani viongozi wao wote wamehamia CCM tayari kutokana na kazi ambazo unafanya,”amesema Sanda

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa upinzani wamekuwa wakihama kutoka katika vyama vyao vya siasa na kujiunga na chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile wanachodai kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli.


from MPEKUZI

Comments