AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Nikabaki nikiwa nipo kimya, kama nimemwagiwa maji ya baridi, swali la kwanza kujiuliza kichwani ni mbinu gani waliyo itumi hadi mimi leo nipo hai.Nikiwa ninaendelea kuliwazia ninalo liwaza nikamuona Olvia Hitler akiwa amesimama nyuma ya Rahma huku macho yake yakimwagikwa na machozi ya damu
ENDELEA
Nikabaki nikiwa nimeduwaa, pasipo kuzungumza kitu chochote, Olvie akaanza kutingisha kichwa taratibu huku machozi ya damu yakiendelea kumwagika kwa wingi, akauinua mkono wake mmoja na kuanza kuniita taratibu, hapa ndipo nilipoiona mkono wake ukiwa umejaa damu nyingi.
“Walipo niambia kwamba umekufa, ikanilazimu kufanya kitu ambacho kingeurudisha uhai wako, kutokana sikuhitaji uweze kupotea kiurahisi maishani mwangu, wakati bado sijaisha nawe vya kutosha”
Hata Rahma alicho kizungumza sikukitilia maanani kwa maani macho, na akili yangu zote zilikuwa zipo kwa Olvia aliye simama nyuma ya mke wangu Rahma.Olvia Hitler akaunyanyua mkono wake wa pili juu na kuendelea kuniita kwa ishara kiasi kwamba nikazidi kuchanganyikiwa kwa vitendo vyake
“Niliamua kwenda, India kwa wanganga wanao tumia nguvu za kienyeji.Ambapo kuna mganga mmoja ambaye ni maarufu sana aliweza kunisaidia sana, hadi akaurudisha uhai wako”
Nikayahamishia macho kwa Raham, kisha nikayarudisha tena macho yangu kwa Olvia Hitler
“Mganga yule, alikupandikiza roho ya nyoka, na kila katikati ya mwaka na mwisho wa mwaka nilazima ugeuke kuwa.......”
Rahma alisita kidogo kuzungumza kitu anacho kizungumza na nikabaki nikiwa nimemtazama kwa umakini
“Utageukuwa kuwa nyoka mkubwa, na ninatakiwa kukupa watu wawili, uwale ili uweze kuongeza maisha ya kuishi la sivyo utakufa kabisa na nitakukosa mume wangu”
Rahma alizungumza huku akimwagikwa na machozi, nikaanza kujitazama kiungo kimoja baada ya kingine kwa maana sikuamini kama hapa mimi nilipo nimekuwa na pumzi ya nyoka.Olvia Hitler akapiga hatua moja nyuma kisha akasogea hatua nyingine moja kushoto, hapo ndipo nikamshuhudia utumbo wake ukiwa umechomoza nje, na ameushika na mkono mmoja ili usiguse chini
“Eddy”
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment