Ndege Tanzania aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imezuiliwa nchini Canada imekwishaondoka kuja nchini

Kwa Mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Gerson Msigwa amesema Ndege ya Tanzania iliyokuwa inashikiliwa nchini Canada imeshaondoka nchini humo na inarejea Tanzania.

Msigwa ameandika hayo kupitia ukurasa wakwe wa mtandao wa kijamii wa Twitter

Pia Msigwa ameongeza kuwa Ndege 3 kubwa, Mbili aina ya Bombardier CS300 kutoka Canada na Moja Boeing 787-8 Dreamliner kutoka Marekani zitawasili baadae mwaka huu


"Ndege yetu aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imezuiliwa nchini Canada ilikwishaondoka Canada kuja Tanzania. Aidha, ndege kubwa nyingine 3 (2 Bombardier CS300 kutoka Canada & 1 Boeing 787-8 Dreamliner kutoka Marekani) zitawasili baadaye mwaka huu. Nawatakia Ijumaa Kuu njema."-Msigwa



from MPEKUZI

Comments