Mpiga picha wa Diamond ajibu kufukuzwa WCB

Baada ya Mpiga Picha wa Diamond Platnumz ‘Kifesi’ kutangaza kuacha kazi hiyo, kumeibuka stori kuwa Kifesi amefukuzwa kazi kitu ambacho amekikanusha vikali.

Kifesi amesema taarifa zinazodai kuwa amefukuzwa kazi hazina ukweli wowote na kilichotokea ni maamuzi yake binafsi.

“Hapana sijawahi kuachishwa kazi, kama niliachishwa basi niliachishwa pasipo kupewa taarifa, ninachofahamu nimechukua maamuzi haya na ni kitu ambacho nilikuwa nimepanga kufanya kutoka siku nyingi, so jana nikasema i think it right time to do this,” Amesema Kifesi

Pia amejibu kuhusu kuingilia masuala ya Diamond na Zari ndiko kumepelekea hayo, Kifesi amejibu; “Kumtetea zari sijaanza leo, ukiangalia Instagram kuna posti za zamani nilikuwa nafanya hivyo lakini ni suala gumu kulielezea”.

Dada wa Diamond, Ema Platnumz baada ya kusikia taarifa za Kifesi kuacha kazi, kwenye moja ya post Instagram ali-comment; “Acha uongo Kifesi umefukuzwa kwa kuacha kazi na kufuatilia maisha ya bosi wako yametushinda sie wee mtu baki utaweza”.


from MPEKUZI

Comments