Kamanda wa Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema wamejipanga vizuri katika kuimarisha hali ya usalama nchini katika sikukuu hii ya Pasaka na kudai atakayethubutu kufanya vitendo vya kiharifu atachukuliwa hatua kali.
Kamanda Mambosasa ameeleza hayo leo (Machi 30, 2018) wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kusema kulingana na uzoefu waliokuwa nao wamejipanga kuimarisha usalama kwa hali ya juu ili wananchi waweze kusherehekea kwa amani na utulivu.
"Jeshi la Polisi litahakikisha wananchi wa Dsm wanasherehekea sikukuu hii kwa amani na utulivu na kwa kuwa uzoefu unaonesha kwamba mara nyingi katika sherehe kama hizi watu wenye nia ovu wanajiandaa kufanya vitendo vya kiharifu ikiwa na pamoja na kufanya ujambazi ili kujipatia vipato kwaajili ya kusherehekea sikukuu", amesema Mambosasa.
Pamoja na hayo, Mambosasa ameendelea kwa kusema "baada ya kulijua hilo Jeshi la Polisi tumejipanga vizuri, kwamba hakuna mtu yeyote atakayeweza kupata fursa ya kufanya lolote katika uvunjifu wa sheria, tumeimarisha doria lakini tunaendelea na misako maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam katika mikoa yote mitatu na wilaya zote za kipolisi 11".
Kwa upande mwingine, Kamanda Mambosasa amesema hayo yote yanafanyika kwa lengo la kuimarisha hali ya usalama katika siku kama hizi za sikukuuu.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment