Idriss Sultani Amchokonoa Wema Sepetu

Mrembo Wema Sepetu ametoa sababu ni kwanini kila mara anapenda kuposti picha za watoto tofauti tofauti katika ukurasa wake wa Instagram.

Ameeleza hayo baada ya kufanya hivyo na baadae mugizaji Idris Sultan kumwambia; si uanzishe tu nursery.

Mrembo huyo aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2006 hakukawia kujibu comment hiyo ya Idriss, ni kama alichokozwa alivyoijibu kwa haraka;

"Dah… mbona ningekuwa nae wa kwangu ningekuwa nampost all the time… ni kwasababu tu sina wangu… so i post every baby dat melts my heart…Since i don’t have one to call my owm… ila ningekuwa nae mbona ungeni-unfollow… Smh…

Utakumbuka mwaka 2016 Idris na Wema walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na ilifikia hatua wakaeleza kuwa wanatarajia kupata watoto mapacha, hata hivyo baadae ilikuja kuripotiwa kuwa ujauzito huo kuharibika.


from MPEKUZI

Comments