Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 05 na 06

 Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA
***ilipoishia***

akanyanyuka haraka akaanza kumkagua kulwa kwa kugisi huenda damu hizo zinamtoka mwanae....alistahajabu kumkuta kulwa hana jeraha lolote.....Rose akaamua kuzipiga hatua za taratibu huku hofu kubwa imetanda juu yake....macho ya Rose yalionekana kutazama kwa tahadhari kubwa.....wakati huo bi'chenda macho yalimtoka akawa na wasiwasi....jasho lilimtoka mfululizo hata hakusikia maumivu ya lile jeraha alilochomwa na kipande cha chupa..
Rose alipokaribia kuifikia kabati,,,ghafla ikasikika Honi ya pikipiki......upande wa nje ya Geti...

***Endelea***
Rose akastuka.....akazipiga hatua za harakaharaka mpaka dirishani, alipochungulia aliona pikipiki nje ya uzio..kutokana geti lilikuwa na uwazi kuanzia katikati mpaka upande wa juu..akamuina Mumewe Seba amerudi...Rose akaamua kutoka chumbani na kuelekea upande wa nje ili akafungue geti....
Bi'chenda akaona hiyo ndio nafasi pekee ya kutoka chumbani humo......akatoka haraka kule nyuma ya kabati,huku akichechemea akazifuta yale matine ya damu iliyokuwa kwenye sakafu.......kisha akafungua mlango alipotoka nje,,,akakutana uso kwa uso na Rose huku akiwa Seba kwenye korido....Bi'chenda alistuka sana..hakutarajia kukutana na Rose akimshuhudia akitokea chumbani kwake..wakati tangu asubuhi alionekana kuwa hayupo ndani ya nyumba hiyo...Rose alistahajabu kumuona mama mke wake akiwa ameva kaniki nyeusi kwa kujifunga rubega.....Seba hakushangaa,, hakujua kilichokuwa kinaendelea ndani ya nyumba hiyo...

Rise akauliza kwa mshangao....Mama ulikuwapi nimekutafuta tangu asubuhi haukuwepo ndani!!!....Bi'Chenda akajibu kwa kudanganya,,huku akitabasamu akasema,,"mimi nilikuwemo chumbani kwangu nimelala najisikia homa,,,nimeamka baada ya kumsikia kulwa akilia...ndio nikawa nimeingia humu chumbani kuona kapatwa na nini,,,sijakukuta..
nimembembeleza amekwisha nyamaza...Rose hakujali akajisemea moyoni,,"kumbe alikuwemo chumbani kwake...mmh!!!niliogopa...
Rose na Seba wakaingia chumbani....



from MPEKUZI

Comments