Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 01 na 02

  Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA
Ilisikika sauti ya mwanamke akilia kwa sauti kali sana ndani ya sekunde chache.....kisha sauti hiyo ikatulia kimya....baada ya sekunde kumi ikasikika sauti ya mtoto mchanga akilia.....baada ya dakika kumi kupita,,zikasikika sauti zikisikika zikisema"sukuma kwa nguvu....usibane mapaja utamuuwa mtoto...ghafla ikasikika sauti ikisema ""mama weee...

baada ya sekunde tatu hivi ikasikika sauti tena ya mtotochanga akilia....mwanamke huyo aitwae Rose alijifungua watoto mapacha wote wa kiume.walipishana dakika kumi za kuzaliwa...Rose alifurahi sana..Akamshukuru Mungu kwa kujifungua salama...baada ya masaa mawili kupita alikuja mumewe aitwae SEBA....alifurahi sana akasema,nitakupa zawadi mke wangu..nakuahidi nitakununulia gari...Rose alifurahi sana kusikia kauli hiyo ya mumewe..

***************
kesho yake majira ya saa nne za asubuhi.. madaktari walimruhusu Rose kwenda nyumbani..kutokana Rose alikuwa na nyonga pana sana hivyo haikuwa vigumu yeye kuzaa.. alijifungua salama bila kufanyiwa upasuaji wala kuongezewa njia kwa kuchanwa ukeni.
Seba alimchukua mkewe pamoja na mama yake mzazi ambayae ni mama mkwe wake Rose wakatoka nje ya hospital,,waliingia ndani ya gari na kuianza safari ya kuelekea nyumbani.

*************
ilipofika majira ya saa saba za usiku....mama yake na Rose aliamka....akanyanyuka kutoka kitandani akafungua begi lake na akatoa kaniki nyeusi akajifunga rubega...kisha akatoa mkoba mdogo uliokuwa umetengenezwa kwa ngozi ya Nyumbu.. akaufungua na kutoa irizi mbili zilizokuwa zimefungwa kamba nyeusi nyemba....akazivaa irizi hizo.....akazipiga hatua mpaka kwenye kona ya chumba akasimama wima. huku makalio kayageuzia ukitani......akatoweka kichawi....akajitokeza ndani ya chumba cha mwanae.....Rose alikuwa kalala fofofo pamoja na mumewe Seba...Mama huyo aitwae Bi'CHENDA  akavua irizi moja yenye rangi nyekundu..akaitemea mate kisha akazipiga hatua kukifuata kitanda...alipofika karibu sana...akaanza kukizunguka kitanda mara tatu..kisha akamgusa pacha mmjoja kichwani kwa kutumia irizi hiyo...akazioiga hatua na kueleke kwenye kona ya chumba hicho akageuka na makalio yakageukia ukutani kisha akatoweka kichawi....



from MPEKUZI

Comments