Polisi yawashikilia watu 10 kwa mauaji diwani wa Chadema Morogoro

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikiliwa watuhumiwa zaidi ya 10 wa mauaji ya aliyekuwa diwani wa Chadema, Kata ya Namwawala Wilaya ya Kilombero, Godfrey Lwena.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa uchunguzi na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Lwena aliuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake akiwa nyumbani kwake Februari 22, 2018.

Matei amesema kwa sasa majina ya watuhumiwa hayo yanahifadhiwa ili kutoharibu uchunguzi, na kwamba yatawekwa wazi baada ya upepelezi kukamilika.

Awali, katika taarifa yake kwa nyombo vya habari kamanda Matei amesema mauaji hayo yanatokana na kisasi kufuatia kifo cha mkazi wa kata hiyo, Kennan Haule aliyeuawa na watu wasiojulikana mwanzoni mwa mwaka 2016.

Amesema mtu huyo ameuawa kufuatia mgogoro wa shamba uliopo kati ya wananchi na Bodi ya Sukari ambapo Lwena alinukuliwa akiwaambia wananchi kuwa Haule asipokufa hawatapata haki yao na baada ya siku kadhaa aliuawa.

Amebainisha kuwa eneo hilo lina migogoro ya muda mrefu ya mashamba na watu wengi wameuawa katika mazingira yanayofanana.

 “Tunaendelea na uchunguzi wa kina katika eneo lile la Namwawala na kata za jirani ili kubaini hao wanaoendesha haya mauaji na wote watachukuliwa hatua za kisheria,” amesema  Matei.


from MPEKUZI

Comments