MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Kuingia ndani kwangu nikakuta simu yangu ikiita na kukuta ni Hassani akinipigia, nikaipokea akanijulisha yupo njiani anakuja, kwa haraka haraka nikajiandaa, nilipo maliza tu akanipigia simu tena na kunifahamisha kwamba yupo nje. Nikabeba begi langu, nikatoka na kufunga chumba changu, nikiwa kwenye kordo nikakutana na Mariam akitoka kuamka huku akiwa amejifunga, tenge moja. Alipo niona kwa haraka akaja kunikumbatia, joto lake likapenya kwenye mwili wangu na kujikuta nikisisimka. Tukiwa bado tumekumbatiana nikasikia mlango wa chumba cha mama Mariam ukifunguliwa, ikionyesha kwamba ndio anatoka chumbani kwake.
ENDELEA
Nikamuachia Mariam kwa haraka na kwaishara nikamonyeshea kwamba nitampigia simu, na asiwe na wasiwasi. Mama Marim alipo fungua mlango, macho yetu yakakutana.
“Mama mimi ndio ninakwenda”
“Ahaaa sawa Dany nakutakia safari njema na ugua pole”
“Sawa mama”
Tulizungumza mazungumzo ya mafumbo, kamba vile ni watu tunao heshimiana kumbe ni masaa machache tu yamepita tumetoka kuburudishana. Nikawaaga wote kwa pamoja yeye na mwanaye kisha mimi nikatoka nje na kumkuta Hassani akiwa ananisubiria nje ya gari. Akanipokea begi langu na kuliweka siti za nyuma. Kutokna gari yenyewe ni VX V8, hakuona haja ya kuliweka begi langu hilo nyuma kabisa kwenye buti. Nikapanda kwenye gari na Hassani naye akaingia, taratibu safari ikaanza. Tukiwa kwenye mataa ya Ubungo, simu yangu ikaita, nikaitoa mfukoni na kukuta ni K2 ndio anaye piga.
“Ndio bosi”
“Mumefika wapi?”
“Ndio kwanza tupo foleni hapa Ubungo mataa”
“Ahhaa sawa, nilitaka kulifahamu hilo tu”
“Usijali”
“Basi safari njema mukifika Tanga utanijulisha”
“Sawa”
Nikakata simu na kuirudisha mufukoni. Magari ya upande wetu yakaanza kuruhusiwa na trafki anaye yaongoza magari sehemu hii. Safari ikaendelea huku kwenye gari tukisikiliza msiki wa taratbu. Kutokana na mikiki mikiki niliyo ipata jana usiku na mama Mariam, nikajikuta nikipitiwa na usingizi na kumuacha Hassani akifanya kazi yake ya uendeshaji, sikuwa na wasiwasi naye kwa maana Hassani ni dereva mmoja mzuri, hadi amepewa jukumu la kumuendesha bosi wa kitengo chetu basi aliweza kufudhu majaribio mengi aliyo pewa kabla ya kuajiriwa.
Kwa mbali nikiasikia sauti ya Hassani akiwa anazungumza na mtu, taratibu nikajikuta nikifungua macho, nikakuta simu yake akiwa ameiweka sikioni. Nikataza nje ya kioo na kukuta tupo Chalinze, kwenye foleni kidogo ya mabasi yaendayo Morogoro na mikoa ya Tanga na Arusha.
“Sawa honey”
Hassani akakata simu, na kuiweka mfukoni mwake.
“Kaka umetembea?”
“Yaaa nimetumia lisaa kama na dakika tano hivi, ingekuwa hii asubuhi hakuna foleni foleni ya mabasi, basi sasa hivi tungekuwa mbali sana”
“Sawa sawa, tukifika pale Lugoba naomba tuingie tupate kifungua kinywa”
“Sawa sawa”
Safari ikazidi kusonga mbele muda huu tukiwa tunazungumza mambo mengi na Hassani. Tukafika maeneo ya Lugoba na kuingia kwenye shele hiyo ambo watu hapa wanajipatia vyakula mbalimbali. Hassani akasimamisha gari pembeni, kisha tukashuka wote wawili, akalifunga na kuelekea katika sehemu yenye mgahawa.
“Hassani zungumza tu unakula nini?”
“Kaka labda chai ya maziwa na sambusa”
“Kula ndugu yangu”
“Ahaa huwa nikiwa ninasafiri tena nikiwa ninaendesha huwa sipendi kula sana, huwa tumbo linamtindo wa kunisumbua sumbua”
“Sawa”
Nikaagizia sambusa tano na supu. Vikaeletwa vyakula hivyo na muhudumu tuliye muagiza na kuanza kula msosi huo taratibu taratibu. Tukiwa hapo mabasi kadhaa yakaingia, huku basi moja linalo kwenda Tanga niliweza kulifahamu, linaitwa Ratco. Wakashuka abiria wake, kwa ajili ya kuweza kujipatia vyakula na kunyoosha viungo.
“Hili gari linakwenda Tanga”
“Ahaaa”
“Yaa kampuni yake ipo maeneo ya uwanja mmoja Tanga uitwa Mkwakwani”
“Ahaa sawa, alafu hizi gari zipo nyingi sana”
“Yaa zipo nyingi”
Tukaendelea kula taratibu huku tukiwatazama abiri wanao zunguka zunguka kwenye sehemu hii, huku wengine wakionekana kuwa na haraka haraka. Gari ambalo tunalizungumzia, likaanza kuondoka eneo hili na kuelekea Tanga. Ila tukiwa hapo, tukamuona dada mmoja, akihaha huku baadhi ya wauza miskaji wakimuuliza ana tatizo gani.
“Ratco imeniacha”
Dada huyo alizungumza huku machozi yakinilenga lenga.
“Ratco si hili basi lililo ondoka muda huu?”
Hassani aliniuliza huku akimtazama dada huyo mwenye asili ya kiarabu.
“Ndio hilo”
“Kama linaelekea Tanga, basi tuondoke naye, tulifukuzie gari hilo”
“Hembu ngoja”
Nikanyanyuka kwenye kiti na kumfwata dada huyo sehemu alipo simama na wauza miskaki hao, wanao onyesha kufanya juhudi za kutaka kumsaidia.
“Samahani dada umechwa na basi hillo linalo elekea Tanga?”
“Ndio kaka yangu naomba munisaidie jamani”
“Mimi nipo na gari binafsi tunaelekea Tanga, tunaweza kulifukuzia gari hilo na kulipata”
“Kaka anga tafadhali nakuomba sana”
Dada huyu aliye valia baibui jeusi, alizungumza kwa kubabaika sana.
“Naomba unisubiri hapa”
Nikarudi hadi kwenye kiti alicho kaa Hassani, nikamuita muhudumu, nikampatia pesa anayo tudai, kisha Hassani akanyanyuka na kuelekea alipo lisimamisha gari. Nikamfwata dada huyo alipo, tukaelekea sehemu gari lilopo, yeye akapanda siti ya nyuma na mimi nikaka siti ya mbele ambapo ndipo kuna nilipo kuwa nikekaa.
“Dada yangu funga mkanda tafahali”
Dada huyo akatii alicho eleza na Hassani, na hapo safari ikaanza. Hassani ikamlazimu kutumia ujuzi wake wote katika kuhakikisha kwamba analifukuzia basi hilo na kulipata. Mara kwa mara nikawa ninayatupia macho yangu kwenye dasbod ya gari hili na kuona jinsi mshale wa spidi unavyo panda taratibu hadi kwenye spidi mia na thelathini. Nilijikuta nikiguna kimoyo moyo kwa maana gari kusema kweli, linakwenda mwendo mkubwa, sikuweza kumuambia Hassani apunguze kwa maana lengo la kufanya hivyo ni kulipata basi hilo.
“Dada usiwe na wasiwasi tutalipata basi hilo”
Nilizungumza huku nikigeuka nyuma na kumtazama dada huyo, anaye onekana kujawa na wasiwasi mwingi sana. Hassani hakuishia hapo akazidi kuongeza mwendo kasi, hadi mapigo ya moyo yakawa yananienda mbio kwani tayari mstari huo ulisha gonga kwenye spidi mia na sabini.
“Hapa tukikutana na askari wakitupiga tochi imekula kwetu”
Hassani alizungumza, huku akilipita gari kubwa, semitrela ambalo nalo lipo kwenye mwendo wa kasi. Hadi tunafika maeneo ya daraja la Wami, kidogo Hassani akapunguza mwendo, kwenye matuta hayo, ila basi hilo hatukuweza kulikuta.
“Ina maana Ratco inakimbia kiasi cha kutowea kulikuta?”
Hassani alizungumza na kumfanya dada huyo ambaye hadi sasa hivi hatulifahamu jina lake.
“Ndio, dereva wa leo anakwenda kasi kama nini?”
“Aahaaa anataka kugeuza tena?”
“Ndi akifika tena Tanga anageuza na kurudi nalo Dar”
“Basi hakuna tabu, hadi tunafika Segere na kuhakikishia Dany, tutakuwa tumesha likuta”
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment