Rais Magufuli Amjulia Hali Mzee Majuto Hospitalini, Afunguka Alivyomtabiria Makubwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtembelea muigizaji mkongwe, Mzee Majuto katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam ambako amelazwa akitibiwa.

Akizungumza mara baada ya kutembelewa na Rais, Mzee Majuto amefunguka na kudai yeye ndio mtu wa kwanza kutabiri ujio wa Rais Magufuli katika kuongoza nchi ya Tanzania huku akisisitiza kwamba anajisikia faraja kuona ana misimamo iliyokuwa imara.

“Mimi ndiyo mtu wa kwanza kumtabiri kwamba akiwa Rais itakuwa shughuli. Nilishukuru sana kuchaguliwa huyu bwana, tumepata Rais sio masihara watu wote sasa hivi wana adabu zao wanajua nini maana ya kazi”, alisema Majuto.

Pamoja na hayo, Mzee Majuto aliendelea kwa kusema ;“sisi wazee tunafarijika sasa hivi, viwanda kila kona vimetapakaa na leo amekuja kutembea hospitalini hapa sijui kama wengine hawajikojolea huko kwa uoga maana hataki masihara. Hii ndio raha ya kupata viongozi wenye msimamo”.

Kwa upande mwingine, Mzee Majuto amesema sio rahisi kupata Rais mwenye misimamo na asiyekuwa na masihara kama Dkt. John Magufuli.


from MPEKUZI

Comments