MBUNGE wa Iramba Magharibi, Singida na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameongoza jahazi la makada, wanachama na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uzinduzi wa kampenzi za uchaguzi mdogo wa ubunge kwa Jimbo la Kinondoni.
Katika uzinduzi huo ambao umefanyika katika Viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam, CCM wamemnadi Maulid Mtulia na kuwaomba wananchi wa Kinondoni wampe kura za kutosha ili aweze kuwawakilisha vilivyo bungeni ikiwa ni pamoja na kutatua kero zao, kushirikiana na serikali bega kwa bega katika kuleta miondombinu ya maendeleo kwa jimbo hilo.
Mwigulu nchemba akizindua kampei za CCM katika Viwanja vya Biafra Kiondoni, Dar.
“Msije mkaenda kupiga kura ya uchaguzi mdogo kwa kiwango kidogo, mkapige kura kwa kiwango cha uchaguzi mkuu, kila mmoja akawe kampeni meneja wa mgombea wetu, aje na wapiga kura siku ya kupiga kura Februari 17, na hiyo ndiyo faida ya mtandao wa chama chetu .
“Sababu zote za msingi za ushindi tunazo sisi, wao wamebaki na hoja moja tu kwamba Mtulia amehama kwa nini? Ilani ya uchaguzi iliyochaguliwa ni ya CCM na itatekelezwa hadi mwaka 2020, asitokee mtu ambaye atawadanganya, kumpigia kura mtu wakati hana ilani inayotekelezeka ni sawa na kupigia kivuli wakati kuna mtu,” alisema Mwgulu wakati akiwasihi wananchi kumpigia kura Mtulia.
Aidha katika mkutano huo, wanachama wengi wa upinzani wamerudisha kadi na kujiunga na CCM.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment