Mbowe: Moleleli ni Daktari Asiye na Uwezo na Alikuwa ni Mtu wa Kujikomba CCM

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amefunguka na kukanusha taarifa alizotoa mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Siha, Dkt Mollel kuwa aliamua kuhama CHADEMA na kwenda CCM kwa kuwa alizuiwa kuongea na viongozi wa CHADEMA.

Mbowe amesema hayo juzi katika uzinduzi wa kampeni za mgombea Ubunge wa CHADEMA katika jimbo la Siha, Elvis Mosi na kudai kuwa Molle hakuwa na uwezo wa kujenga hoja na ni mtu ambaye amekuwa akijikomba kwa watu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

"Mollel hajazuiliwa na mtu bali ni Dk. asiye na uwezo, hana uwezo wa kujenga hoja ni mwanaume anajikomba komba kwa watu wa CCM

".... niwambie watu wangu wa Siha mnapokuwa mnachagua viongozi sisi kama chama tunawapima kila mwaka, huyu uchaguzi unaokuja ataturudishia jimbo au atatunyima jimbo? 

"Na kwa vigezo mbalimbali vya chama vilivyofanyika wananchi wa Siha mshukuru kwa sababu mlikuwa unatuchagulia gunia la misumari bila kujua, angebaki kwa miaka mingine mitatu kwenye nafasi yake ya Ubunge CHADEMA wananchi wa Siha mngeichukia" alisema Mbowe

Mbowe aliendelea kusisitiza kuwa kitendo cha Mollel kujivua uanachama na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge jimbo la Siha ni mpango wa Mungu na ni jambo zuri kwani lingefanya chama hicho kuchukiwa na wananchi.

"Huu ni mpango wa Mungu aliona wananchi wa Siha nikiwaachia hili gunia la misumari litakuwa si jambo zuri hivyo akamtia uchizi akaamua kuhama chama, kwa hiyo hatuna cha kulia kila kitu ni mpango wa Mungu, alijua kwamba Siha tumejitwisha gunia la misumari"


from MPEKUZI

Comments