Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Ndugu Dorothy Semu, anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika mikoa mitano ya Tanzania Bara akiambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho.
Ziara hiyo ya siku nane itaanza tarehe 30 Januari 2018 hadi Februari 6, 2018 kwenye mikoa ya Kahama ambao ni Mkoa Maalum wa Kichama, Kigoma, Katavi, Shinyanga, Tabora na Kigoma.
Aidha taarifa ya Chama hicho imebainisha kuwa katibu ataambatana na Ndg. Wilson Mshumbusi ambaye ni Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee Taifa, Ndg. Janeth Rithe ambaye ni Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa pamoja na Katibu wa Sera na Utafiti Ndg. Idrisa Kweweta.
Moja ya majukumu ambayo Dorothy Semu atayafanya ni kukagua uhai wa Chama, kutoa maelekezo ya ujenzi wa chama, kusikiliza Kero na changamoto za wanachama na kuzipatia ufumbuzi.
Mbali na hayo Katibu Mkuu huyo pia atakagua maendeleo ya zoezi la uchaguzi wa ndani ya chama. Ziara hiyo pia imeelezwa kuwa itawalenga wanachama na viongozi wa ACT Wazalendo wa maeneo hayo.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment