Waziri Simbachawene Aongoza Kikao Cha Mawaziri


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameongoza kikao cha Mawaziri kwa lengo la kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za makazi.

Kikao hicho kimefanyika Mei 27, 2022 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma ambapo kilihudhuriwa na mawaziri wakiwemo  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Nchi Ofisi wa Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angelina Mabula.

Kikao hicho kimefanyika kama sehemu ya maandalizi ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti  2022 nchini  ambapo itakuwa Sensa ya Sita tangu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 na  sensa ya watu na makzi hufanyika  kila baada ya miaka 10.



from MPEKUZI

Comments