Serikali yapokea mapendekezo ya wananchi wa Ngorongoro


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea mapendekezo kutoka kwa wananchi wa tarafa za Loliondo, Ngorongoro na Sale kuhusu namna bora ya kulinda uhifadhi wa maeneo hayo.
 
Mapendekezo hayo yamewasilishwa kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma na wawakilishi wa wakazi wa wilaya hiyo wakiwemo mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Shangai, Malaigwanani, Madiwani, wenyeviti wa vijiji, wawakilishi wa wanawake na vijana.
 
Baada ya kupokea mapendezo hayo, Waziri Mkuu Majaliwa amewasisitiza wananchi hao waendelee kuiamini serikali kwani haiwezi kuwa na mipango mibovu kwa wananchi wake.
 
Akizungumzia kuhusu eneo la Msomera lililoko wilayani Handeni mkoani Tanga ambako yanaandaliwa makazi kwa ajili ya kuwahamishia wakazi wa Ngorongoro waliokubali kuhama kwa hiari amesema, ujenzi unandelea vizuri.
 
Amesema ujenzi wa nyumba za makazi 103 upo mbioni kukamilika na pia serikali imepanga kuongeza nyumba nyingine lengo likiwa ni kufikia nyumba 500 kwa ajili ya wakazi hao.


from MPEKUZI

Comments