Putin: Yeyote Atakayeingilia Mzozo Wa Ukraine Atapata Pigo La Kihistoria


Baada ya kutangaza mashambulizi dhidi ya Ukraine, Rais wa Urusi, Vladimir Putin ametoa onyo kwa Mataifa ya Magharibi kuingilia kinachoendelea baina ya Nchi hizo.

Mara baada ya milipuko kuripotiwa katika Mji Mkuu wa Ukraine, Kyiv Putin alinukuliwa akisema, “Kwa yeyote atakayeingilia kutoka nje, atakutana na matokeo ambayo hajakutana nayo katika historia…”

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliitisha Kikao cha Dharura mara baada ya Urusi kuanza mashambulizi.


from MPEKUZI

Comments